Sunday, March 4, 2012

ASKOFU AFUNGISHWA NDOA NA MAMA YAKE MZAZI:

 Askofu Mkuu wa Kanisa la Pentekoste la Welfare Ministry of Africa, Stanley Mnai akivikwa pete ya ndoa na Bibi Harusi, Gloria Kaserwa katika kanisa hilo lililopo eneo la Vetenari, Temeke jijini Dar es Salaam wiki iliyopita. Katikati ni Askofu Msaidizi, Upendo Mnai, ambaye ni mama mzazi wa bwana harusi. Na Mpiga picha Maalumu
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Kipentekoste la Welfare Ministry of Africa, Stanley Mnai amefungishwa ndoa takatifu na mama yake mzazi ambaye pia ni Askofu Msaidizi wake, katika misa ya 40 Kibaha ndoa iliyofanyika makao makuu ya kanisa hilo lililopo eneo la Vetenari, Temeke jijini Dar es Salaam.

Kanisa hilo lililoanza rasmi mwaka 2009 na kuvuta waumini wengi, lina viongozi wawili tu wenye vibali rasmi vya kufungisha ndoa takatifu kanisani hapo, ambao ni Askofu Mkuu na Askofu Msaidizi.

Kwa sasa, Askofu Msaidizi ni mama mzazi wa Askofu Mnai aitwaye Upendo Mnai ambaye
alifungisha ndoa hiyo ya kwanza Jumapili iliyopita tangu awe askofu msaidizi, huku kukiwa na mahudhurio ya waumini wengi, wakiwamo ndugu, jamaa na marafiki wa maharusi.

Mvuto wa ndoa hiyo ya Askofu haukuwa kanisani tu, bali ulianzia wakati wa maandalizi, kwani tofauti na yalivyo mazoea ya kuona bibi harusi mtarajiwa akiandaliwa sherehe ya 'Kitchen Party’ na upande wake, hali ilikuwa tofauti kwa ndoa ya Askofu Mnai, kwani mama mkwe wa bibi harusi mtarajiwa, Gloria Kaserwa ndiye aliyeandaa shughuli hiyo kwa ajili ya binti anayetarajiwa kuolewa na mwanawe.

No comments:

Post a Comment