Thursday, August 25, 2011

RAIS KIKWETE AMSIMAMISHA KAZI KATIBU MKUU WIZARA YA NISHATI NA MADINI,DAVID JAIRO:

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw David Jairoalipokua anazungumza na Waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuripoti wizarani jana.

Wafanyakazi kutoka Idara ya Nishati iliyopo chini ya Wizara ya Nishati na Madini wakilisukuma kwa nyuma gari lililokuwa limembeba Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw David Jairo mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Wizara hiyo mapema jana asubuhi.
Habari toka Bungeni Mjini Dodoma zinasema Rais Jakaya Kikwete ameamuru  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini  Bw David Jairo asiendelee na kazi hadi hapo baada ya uchunguzi dhidi yake wa kuchangisha pesa ili Bajeti ya wizara yake ipite ukamilike.

Hayo yamesemwa sasa hivi na Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda wakati akijibu swali la papo kwa hapo toka kwa Kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai Mh Freeman Mbowe, ambaye alitaka kujua kama Bw. Jairo ataendelea kuwa likizo ili kupisha mchakato wa uchunguzi huo utaofanywa na kamati teule ya Bunge.

"Jambo hilo limekwisha fanywa na Mheshimiwa Rais", alijibu Mh Pinda kwa utulivu na kwa kifupi baada ya swali hilo,huku wabunge wakishangilia kwa kugonga meza. Hatua hii inakuja siku moja tu baada ya Bw. Jairo kuripoti ofisini kwa shangwe, ambapo wafanyakazi wa wizara walimpokea kwa vifijo, na wengine hata kusukuma gari lake hadi ofisini, aliporipoti mapema asubuhi.

Uamuzi wa kumrejesha kazini Bw Jairo ulipokewa kwa husia tofauti na  kila kada nchini, wengi wakihoji sababu ya mhimili mmoja kati ya mitatu iliyopo (Serikali, Bunge na Mahakama) kuingilia mwingine, ikizingatiwa kamba sakata hilo liilianzia bungeni na wengi walihisi ingekuwa vyema Bunge lingelishughulikia hadi mwisho.

Bunge liliridhia kuundwa kwa kamati maalumu kuchunguza tuhuma hizo na  inategemewa wajumbe wake watatangazwa kesho wakati wa kufunga kikao cha  Bunge kinachoendelea sasa. Ripoti yake inategemewa kutolewa Bunge lijalo.

No comments:

Post a Comment