Sunday, June 3, 2012

HOTUBA YA NAIBU WAZIRI WA ELIMU ALIPOFUNGA CLINIC YA SPRITE HASHEEM THABEET 2012:

Mhe. Phillipo Mulugo (MB)Naibu Waziri wa Elimu akisoma hotuba yake
 Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa kikapu Tanzania, Phares Magesa,
(Wa Pili Kulia, Brand Manager msaidizi wa Coca Cola Bibi Warda Kimaro(Wa Kwanza Kushoto)A fisa Utamaduni, Ubalozi wa Marekani,  Danna Banks(wa kwanza Kulia),Brand Manager msaidizi
 wa Coca Cola  Bibi Warda Kimaro(Wa Kwanza Kushoto), Hashim Thabeet(Wa Pili Kushoto)
 Baadhi ya Vijana Walioshiriki Clinic Ya Sprite Hasheem Thabeet 2012

Mkurugenzi wa Michezo
Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa kikapu Tanzania Ndugu 
Phares Magesa
Afisa Utamaduni, Ubalozi wa Marekani, Danna Banks
Brand Manager msaidizi wa Coca Cola Bibi Warda Kimaro
Hasheem Thabeet ,
Viongozi wa TBF,
Makocha, 
Wachezaji
wadau wote wa michezo.

Kwa niaba ya Serikali na kwa niaba yangu binafsi napenda kuchukua nafasi hii 
kuwashukuru TBF kwa kazi kubwa walioifanya ya kuakikisha mafunzo haya
 yanafanyika   katika kiwango kizuri , zaidi napenda kuwashukuru Coca cola kupitia 
kinywaji cha Sprite kwa kuendelea kufadhili mchezo wa Mpira wa kikapu hasa katika 
ngazi ya Vijana wadogo, pia nawashukru sana watu wa Marekani kupitia Ubalozi wao
 hapa Dar Es Salaam kwa kusaidia kuendeleza vijana wetu kupitia mchezo wa kikapu.

Kipekee na penda kumpongeza Hasheem Thabeet kwa kuonyesha thamani yake katika
 mchezo wa Mpira wa Kikapu na kukubali kutumia muda wake kwa ajili ya Vijana 
wadogo  kuwapa mafunzo na kuinua ari kwa vijana wetu  ili nao wapate kuwa na ndoto
 na  kufika pale alipo yeye

Nimatumaini yangu mafunzo haya mmeyapokea vizuri mtayazingatia na mtakapo rudi 
kwenye shule zenu nanyi mkawe mabalozi wazuri na walimu kwa wenzenu ambao 
hawakupata nafasi kama hii mliyoipataMikoa iliyoshiriki kliniki hii ya mwaka huu ni 
Mwanza, Tanga, Dodoma,Kilimanjaro, Arusha, Unguja, Pemba na mkoa mwenyeji wa
 Dar es Saalaam hivyo basi ni matumaini yangu mwakani mikoa yote ya Tanzania bara
 na visiwani itashiriki, naomba wafadhili wajitokeze zaidi kuunga mkono jitihada za Cocacola na Hasheem Thabeet ili tuibue vipaji vingi zaidi katika kikapu.

Ndugu zangu serikali ipo pamoja nanyi katika michezo  kama mnavyofahamu wote
 kuwa mashindano ya Umiseta na umitashumta yamerudishwa rasmi mashuleni,   
hivyo mafunzo haya waliyopata vijana hawa basi yatasaidia kuwaimarisha kimbinu za 
kimchezo na ni matumaini yangu mikoa iliyoshiriki hapa itafanya vizuri kwenye 
mashindano yajayo ya shule za sekondari na msingi.

Serikali itaendelea kushirikiana na vyma vya michezo vyote nchini katika kuhakiksha
 michezo inaimarika mashuleni ikiwa ni pamoja kupeleka walimu wengi zaidi 
wakasomee  taaluma hii katika vyuo vyetu mbali mbali, ikiwa ni sambamba na kuongeza 
uwezo wa vyuo vyetu vya ualimu  kufundisha michezo.

Narudia tena wito wangu kuwa michezo ni sehemu muhimu ya kujenga vijana wetu
 kiafya, kielimu na kimaadili na hata kiuchumi hivyo basi ni jukumu la kila mmoja wetu, 
wanamichezo, wazazi, walezi na wakuu wa shule zote nchini kuhakisha vijana 
wanapatiwa fursa ya kushiriki katika michezo.

Nafahamu kuwa changamoto ya miundombinu ya michezo bado ni tatizo kubwa katika
 nchi yetu, hivyo basi Serikali itafanya kila jitihada kushirikiana na wadau wengine 
kuhakikisha tatizo hili linashugulikiwa ipasavyo katika ngazi zote.

Maombi yenu kwa serikali ya kuomba mpewe kipaumbele katika ujenzi wa uwanja
 mkubwa wa ndani wenye hadhi ya kimataifa kama wezenu wa soka na riadha 
wanavyofaidika na uwanja mkuu wa Taifa, nimeyachukua na nitayafikisha katika ngazi 
husika ili yaweze kushugulikiwa.

Nawashukuru sana wadhamini wa mafunzo haya kampuni ya Cocacola kupita SPRITE
 naHasheem Thabeet na nitoe wito kwa wanamichezo wengine Tanzania kuiga mfano 
wa Hasheem Thabeet wa kurudisha fadhila kwa jamii nzima ya watanzania na nia yake
 njema ya kuona vipaji vingine vinaibuka Tanzania.
Niwatakie heri katika mafunzo mengine kama haya yatakyofanyika Arusha juma lijalo.
Natoa wito tena kwa makampuni mengine yajitokeze kudhamini michezo na hususani 
mchezo wa kikapu.
Niwatakie Safari njema wale wote watakaosafiri kurudi mikoani na niwashukuru wote
 kuanzia Walimu wenu,Wazazi kwa kuwapa ushirikiano mzuri katika kuchangia kufanikisha 
malengo yenu.

Asanteni kwa kunisikiliza na sasa nimeyafunga rasmi mafunzo haya ya  
SPRITE HASHEEM THABEET CLINIC 2012.

Mhe. Phillipo Mulugo (MB)
Naibu Waziri wa Elimu

No comments:

Post a Comment