Wednesday, February 29, 2012

P-FUNK 'MAJANI' APATA MTOTO WA KIKE:

Mkurugenzi wa Bongo Records Studio na Mtayarishaji wa siku nyingi wa mziki, Halfan 'Majani-P Funk' (pichani), amebarikiwa kupata mtoto wa kike baada ya mkewe kujifungua salama hospitali alikokuwa amefikishwa. Anasema challenge kubwa ambayo anayo hivi sasa ni kumpatia jina mwanawe huyo wa kike ambapo alitoa wito kwa mtu yeyote yule aliyekuwa tayari kumsaidia kwenye zoezi hilo ilimradi tu jina hilo atakalopendekeza lianzie na herufi P kama ilivyokawaida kwa watoto wake waliotangulia yaani Patricia, Paul/Peter. P-Funk anamshukuru sana mwenyezi Mungu kwa kuweza kumpatia mtoto wa 4 na wala hajutii mtoto huyo kuzaliwa leo tarehe 29 February 2012 eti kisa tu mwanawe huyo atasherehekea tena Birth Day yake nyingine tarehe 29 February 2016 kwasababu ya ukweli kwamba tarehe hiyo hutokea mara moja tu kila baada ya miaka 4. P-Funk aliyasema yote hayo katika kipindi kidogo cha 'You Heard' kama sehemu ya kipindi cha XXL cha Clouds Fm Radio.

No comments:

Post a Comment