Monday, October 31, 2011

ALICHOKISEMA MBUNGE WA ARUSHA MJINI (CHADEMA) MH.GODBLESS LEMA KWA WAANDISHI WA HABARI:

Mbunge wa Arusha mjini (CHADEMA) Mheshimiwa Godless Lema.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Nawasalimu nyote.
Nimewaita kutoa taarifa juu ya kilichotokea juzi tarehe 28/10 /2011 baada ya kuhairishwa shauri la kesi ya uchaguzi iliyoko mahakamani dhidi yangu .Tarehe 27/10/2011 kesi hii ilihahirishwa na Judge A . Mujuluzi kwani usikilizaji wake usingewezekana kwa kuangalia idadi ya watu walivyokuwa wamejaa pale mahakamani ,maagizo yalitoka kwamba shauri litakalofuata mahakama iwe imetayarisha vipaza sauti kwa ajili ya usikilizwaji wa kesi hiyo.

Lakini kwa bahati mbaya jambo hilo halikuwezekana kabisa kwa sababu ambazo baadaye Mh. Judge alizitolea ufafanuzi mzuri na mawakil wa pande zote wakakubaliana kuendelea na shauri hilo bila vipaza sauti lakini kwa ahadi kuwa mpango huo unatekelezwa haraka na wakati mwingine wa kesi itakapokuja mahakami utaratibu huo utakuwa umekamilika.
Jambo la kushangaza siku hiyo wakati nafika mahakamani nilikuta polisi wengi sana na wamevaa nguo zinazoashiria tayari wako kwa mapambano na watu wakizuiwa kabisa kuingia mahakamani kuanzia geti kubwa na polisi walikuwa wanajaribu kuhoji kila mtu kuwa anakwenda kusikiliza shauri gani na kama mtu angejibu ni shauri la kesi ya uchaguzi basi halikuwa haruhusiwi kuingia mahakamani kuanzia geti la mwanzo wa mahakama.

Nilikata dhambi hii na uonevu huu kwa wapiga kura wangu nilimfuata OCD Bwana Zuberi Mwombeji kuongea naye juu ya jambo hili la kuzuia watu na alikataa kabisa na kusema “ hao watu wanaenda wapi kwani kesi inawahusu ? na yeyote atakaye vuka hawa polisi hapa hatakuwa chambo na kuniambia kuwa hata watu wakija maelfu na maelfu mahakamani lazima kesi hii initie kidole “ ( Zuberi) , tulibishana huku nikijaribu kutetea utu wangu na mamlaka yangu kama Mbunge , ikawa zogo mahakamani muda mrefu bila mafanikio mpaka nilipomuomba wakili wangu aingilie kati kisheria ndipo watu waliporuhusiwa kwenda kusikiliza kesi .

Baadaye baada ya kesi nilikuta wananchi waliokuwa nje ya chumba cha mahakama wakiwa na hasira huku wakilalamika na kwani kwa mara nyingine tena OCD Zuberi alikuwa amewaita tena wananchi PANYA na akiamuru polisi wa ngazi ya chini kwa kusema “sogezeni hao PANYA nyuma”Lugha hii ni mbaya haikubaliki hata kidogo, niliongea na wanachi na na kukemea lugha hii kwa hasira baadaye nilielekea ofisini kwangu kwa miguu huku nikisindikizwa na polisi na watu wengi waliokuwa mahakamani na baadhi ya watu niliomba tukutane nao ofisini kwangu wengi wakiwa ni viongozi wa matawi na vijana naotarajia kuwa mashaidi katika kesi ya uchaguzi,niliongea nao ofisini kwangu nikawaaga nikaondoka na wachache niliwaacha ofisini kwangu na Katibu wangu na baadhi ya wageni wengine,baada ya muda nilipigiwa simu kuwa polisi wameingia ofisini kwangu na kukamata watu wote , nilimpigia simu Kaimu RPC kumueleza suala hili nayeye alisema ni bora nifike ofisini kwake tuongee jambo hili ,nilipofika nilimueleza jinsi OCD anavyoendelea kufanya kazi kibabe, kwa shuruti za siasa na bila busara na kuhumiza watu bila sababu , alinisikiliza kwa muda usiopungua saa nzima na baadae nikifikiri nimeeleweka ghafla niliwekwa chini ya ulizi na kuambiwa nitoe maelezo na kushitakiwa kwa kosa la kuongea watu nje kabisa ya viwanja vya Mahakamani na ofisini kwangu .

Ninafahamu mipango yote ya siri na wazi iliyokusudiwa kwangu na wafuasi wangu , ndio maana sishangai kwamba vyama vingine vinaweza kufanya mikutano na maandamano bila kibali na kuchungwa na polisi na yeye OCDna polisi walipohojiwa na waandishi wa habari juu ya jambo hilo UVCCM kufanya mkutano na maandamano bila kibali,, Polisi walisema wanataarifa na wametoa onyo kwa viongozi waliohusika.

Lakini mimi Mbunge nimekatazwa hata kutembea kwa miguu kutoka mahakamani na ni lazima nipande gari hata kama nataka kutembea kwa miguu na hata kuongea na Wananchi mahakamani na ofisi kwangu ni kufanya mkutano bila kibali ? Jambo hili limenisikitisha sana lakini moyo wangu huko imara kwani naamini kila matatizo yanayotokana na kupigani haki au usawamatatizo hayo mara nyingi huwa ni mpango wa Mungu juu ya kusudi Fulani.

Kesi ya uchaguzi bado inaendelea, nilichaguliwa kwa kupata kura zaidi ya elfu 56. Wakija takribani asilimia kumi tu ya walionichagua ni watu zaidi ya 5,600. Watu hawa wakija kusikiliza kesi na baada ya kesi wakaamua kuondoka kwa kuelekea mjini na sehemu mbali mbali , je kundi hili la watu wataondokaje mahakamani ili msongamano huu usiitwe maandamano ? Hatuhitaji nguvu kubwa ya jeshi la polisi kutawanya watu wanaotoka mahakamani tunahitaji ulinzi wao na busara zao ili watu wasambae kwa amani “kwani kusudi la mkusanyiko huu hautokani na nia mbaya bali ni kesi ya uchaguzi ambayo hauwezi kushanga kwanini kuna watu wengi mahakamani.

Matukio mengi ya uhalifu Tanzania huwa yatokei kukiwepo na msongamano wa watu tu bali yanatokea tu pale penye dhamira ya uovu bila hata msongamano,mara nyingi tunasikia taarifa za mabenki kuibiwa , watu kuvamiwa katika nyumba zao usiku na kuchomwa visu na kuporwa mali zao mambo haya huwa yanafanyika tena msongamano wa watu ukiwa usingizini, sio kweli kuwa kila msongamano wa watu ni maandamano au ishara ya vita na uovu ndio maana sokoni na sehemu za ibada huwa hakuna polisi wanaolinda kuepusha msongamano kwani kusudi la msongamano huo unajulikana maudhui yake. Haitoshi kutembea kwa miguu idadi kubwa ya watu kuita maandamano. Maandamo yanatafsiri pana sana.

Hakuna shaka ni siasa ambayo iko wazi juu ya kilichotokeatahere 28/10/2011 kwani sio mara ya kwanza kutoka mahakamani kwa miguu na kuja ofisi kwangu kwani tarehe 21/10/2011 tulitoka mahakamani kuelekea Ngarenaro kwa miguu tena kupitia njia ya polisi , mbona siku hiyo kutembea huko hakuitwa maandamano ? ama kwa vile OCD hakuwepo ? .
Ninatoa wito kwa serikali na viongozi wa jeshi la polisi sio afya hata kidogo mwakilishi wa wananchi kama mimi kuwa na uhusiano mbaya na Jeshi la polisi kwa sababu ya mtu mmoja.

Ndugu wananchi na wanahabari Wakati Fulani huko Nyuma OCD alituma kwa katibu wetu wa Mkoa Meseji kuwa mimi Mbunge nimeandaa mpango wa kumteka mtoto wa OCD na kumuua,Mimi pamoja na Mkiti wetu wa Taifa Mh Mbowe tulienda kumuona RPC na viongozi wengine kujadili na RPC alihaidi na kuona umuhimu wa kukaa pamoja na kujaribu kutafuta uhusiano mwema na suluhu jambo ambalo halikuwezekana mpaka leo kwa sababu pengine za msingi.
Sasa najiuliza nikiwa nimevamiwa usiku au nahitaji polisi kwa msaada wowote ule , je nitakuwa na ujasiri gani wakumuita OCD kwa msaada , kwangu mimi hofu niliyonayo dhidi yake kama kiongozi wa polisi ni kubwa kuliko kukutana na majambazi usiku, hata hivyo” LETS GO, LETS GOD”Lakini kutafakari kwangu historia mara kwa mara inatia moyo kwamba hakuna harakati ambazo hazikuitwa ukorofi ,uvunjaji wa sheria , uhaini, na ukiukwaji wa taratibu , niweke wazi kwamba nitapinga ukandamizaji wowote ule mbele ya yoyote Yule mwenye silaha yoyote ile na mwenye magereza yenye mateso makali kuliko jehanamu bila woga , na sheria yeyote inayokiuka misingi ya Kwa kweli nimejiandaa hata kupokea mauti  japo najua Mungu anapenda niishi muda mrefu ili kutimiza kusudi lake , sitarudi nyuma katika harakati hizi za kupinga uonevu ,dhuluma na ukandamizaji wa haki za binadamu nasubiri kwa hamu sana kuona mikakati yote iliyopangwa kinyume nami na wafuasi wote wanaopinga uonevu. Hata hivyo Nimeiandaa familia yangu kuwa tiyari wakati wowote kwa jambo lolote na kwa taarifa yoyote dhidi ya ukweli tunaoupigania.

Ndugu wanahabari 

kila mara huwa nawaambia wananchi kuwa dhambi mbaya kuliko zote Duniani ni UOGA. Lazima watambue kuwa wengine watateswa ,wengine watauwawa lakini wengine watafurahia haki na uhuru kamili tunaoupigania hata kama hatutakuwepo kwa sababu tu wengine walipitia mateso mbali mbali. Mimi natambua kuwa faida ya kuishisio kuishi vizuri tu wewe na familia yako bali ni wewe kuwa sehemu ya mabadilikio ya watu wanaokuzunguka , katika kupigani UTU ,HAKI ,ustawi mzuri wa Jamii. Na kila mtu anayemuogopa Mwenyezi Mungu ataishi kufanya hivyo kama Mahatma Gadhi alivyopata kusema

 “The best way to find yourself is to loose yourself in the service of others”

Godbless Jonathan Lema (MB)
30/10/2011 .

No comments:

Post a Comment