Thursday, October 18, 2012

JINSI MASKANI MAMA YA CCM-KISONGE-ZANZIBAR ILIVYOCHOMWA MOTO :



Wafanyakazi wa Kikosi cha Zima Moto wakijitahidi kuuzima moto uliokuwa ukiwaka ndani ya Jengo la Maskani ya kisonge lililochomwa moto na watu wanaodaiwa ni wafuasi wa Sheikh Faridi wakisindikiza kuachiwa kwa Sheikh wao huyo ambae wanadhani amekamatwa na Polisi baada ya kutomuana kwa siku Nzima,Jeshi la Polisi limekanusha kumkamata Sheikh huyo na kuwaomba wananchi kushirikiana kumtafuta
 
   Tukio la kuchomwa Moto Maskani ya CCM Kisonge limesababisha pia mali na baadhi ya Vyombo vilivyokua hapo kuteketea kwa Moto kama inavyoonekana Vespa iliowekwa eneo hilo ambayo mmiliki wake hajajulikana ikiteketea.
 
Jeshi la Polisi lilionekana likifanya Doria katika sehemu hio ilikuweka hali ya Usalama.Picha na Yussuf Simai-Maelezo-Zanzibar.

No comments:

Post a Comment