Wednesday, February 29, 2012

SAFARI YA 50 CENT NDANI YA AFRIKA IMEMFANYA AREKODI 'NGOMA' MPYA:

50 Cent hivi karibuni alikua nchini kenya pamoja na somalia kwa ajili ya kutembelea na kuona hali ya wahanga wa njaa akiwa na mpango wa kutokomeza njaa amesema safari hiyo imemfanya aweze kuingia booth na kutengeneza pini jipya (wimbo mpya). Nimeweka kipande cha experience lakini ni kipande kidogo kinachokutaka kusikiliza kwa umakini kuelewa ninachokimaanisha, na nimefanya hivyo kiubunifu ili mtu akisikiliza  aburudike kwanza halafu atafakari.
World Food Program (WFP) ilipomdondosha Fiddy (50 cent), kibera na Somalia, kuangalia kwa mara ya kwanza vita dhidi ya njaa.


"Ninachokiona kinashtua sana, hawa kina mama na watoto, wamerisk kila kitu na kuja hapa kutafuta chakula" alikaririwa Fiddy a.k.a 50 Cent.


Akiwa katika moja ya shule huko kibera (kenya).

Safari iliyomleta ni moja tu ya kujitolea kwa kutoa msaada wa chakula kwa wenye matatizo ya njaa. Kwa kila chupa moja ya kinywaji cha SK (Street King) inayotoka, Fiddy, anachangia kupitia WFP sent 10 za kimarekani.

No comments:

Post a Comment