Wednesday, January 25, 2012

WHAT SO SPECIAL WITH MONALISA..?

Msanii wa filamu ambaye anatikisa hapa nyumbani na hata kimataifa pia (Yvonne Cherryl 'Monalisa'),ameweka wazi kile kinachompa sifa za yeye kufanya vizuri kwenye sanaa ya filamu hadi kufikia kwenye ngazi za kimataifa.Mona ambaye ndi msanii wa kike wa Kitanzania anayeongoza kwa kushiriki kwenye tuzo nyingi za kimataifa kwenye nchi mbalimbali alisema kuwa Heshima na Nidhamu kwenye kazi yake ya filamu na hata nje ya kazi hiyo ndio kitu kinachomfanya yeye akubalike kimataifa na pia ubora wa kazi zake."Unajua mimi sina skendo chafu na wala sivai hivyo vinguo vya nusu uchi ili kujitafutia umaarufu na ndio maana naheshimika hadi sasa" alisema Mona, pia aliongeza kuwa wasanii wengi wa hapa nchini wanafanya kazi za filamu lakini hawatakuja kupata tuzo kwani tabia zao za ndani ya filamu na hata maisha yao ni mabaya.

No comments:

Post a Comment