Marehemu Steven Galinoma
--
Aliyewahikuwa mbuge wa Kalenga, Iringa, Steven Galinoma, amefariki dunia Leo mapema, Taarifa kamili imedhibitisha kuwa mheshimiwa Galinoma amefariki Dunia leo asubuhi mjini Iringa ndani ya gari akiwa anaperekwa hosptalini kutoka kalanga, ambako alikokuwa anaishi. Mheshimiwa Galinoma, alikuwa mtumishi wa serikali mstaafu aliyeshika nafasi mbali mbali katika uhai wake zikiwe Katibu mkuu idara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa, mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa mbuga za wanyama poli,mwenyekiti wa bodi ya mashirika ya Umma(SCOPO),Katibu wa tume ya uchunguzi wa viongozi,pia amewahi kuwa mbunge wa jimbo la Kalenga ,Iringa Marehemu Mhe.Bw.Galinoma alikuwa anaugua kwa mda mrefu pia aliwahi kuenda India kwa matibabu alikua huko wiki 6, na alipata nafuu kwa kiasi fulani lakini baadae alizidiwa tena. Marehemu ameacha wajukuu na watoto ,miongoni mwa watoto wa wake ni wanamuziki Innocent na Buti Jiwe aka Enry Galinoma.
Taaritibu za mazishi zitatolewa si muda mrefu. Mungu amlaze mahala pema peponi.
Kwa habari zaidi za msiba wasiliana na
Joseph Galinoma
00255716492048
Denis Galinoma
00255784769945
No comments:
Post a Comment