Wednesday, January 25, 2012

FACEBOOK YASABABISHA KIFO:

Msichana mmoja huko nchini Nigeria ameripotiwa kufariki dunia baada ya kukatwakatwa na mapanga na mtu aliyedaiwa kuwa ni mpenzi wake wa siku nyingi.Tukio hilo limetokea baada ya mrembo huyo kuanzisha mahusiano mapya na kijana mwingine raia wa Marekani kwa njia ya mtandao wa facebook ambapo penzi liliponoga walikuwa wakikutana hotelini nchini Nigeria ambako kijana huyo huwa anaenda kwa ajili ya kukutana na mrembo huyo.
Mrembo huyo enzi za uhai wake.

Lakini baadae mpenzi wa awali wa mrembo huyo ambaye walipanga kufunga ndoa aligundua mchezo huo na siku walipopanga kukutana tena hotelini hapo, mchumba wa marehemu ambaye pia ni raia wa Nigeria alivamia hotelini hapo na kuanzisha ugomvi,l akini baadae waliporudi nyumbani ndipo mrembo huyo alipomtamkia waziwazi kwamba yeye hamtaki tena.Siku chache baadae baada ya kutamkiwa hivyo kijana huyo alimteka mpenzi wake huyo na kutokomea nae na baadae ikagundulika kuwa alimkatakata kwa mapanga hadi kifo chake.( majina ya wahusika wote hayakuweza kupatikana kutoka kwenye chanzo chetu cha habari).

2 comments: