Kama kawaida wadau wangu nilivyowahidi kuwa nitawaletea matukio ya huku niliko, Cha kwanza kabisa nimekuja huku kwa ajili ya kuongeza vifaa vya kampuni ili mwaka huu tufanye mapinduzi makubwa katika tasnia yetu. Mimi sisemi sana wewe mwenyewe utajionea mambo yatakavyobadilika mwaka huu,pili kuna sinema nayotegemea kupiga katika nchi hizi tatu nilizowatajia China,Hong Kong pamoja na Thailand katikati ya mwaka huu, twende pamoja.
Hapa nikiwa na mshikaji wangu Choba katika maswala mazima ya kununua camera za still picture.
Hapa pia nikiwa na kijana wangu Kounja, huyu kijana jamani hachagui chakula chochote yeye poa tu mpaka supu ya nyoka kijana twende ni hatari sana huyu kijana cheki anvyonikata jicho.
Hili ni soko kubwa la simu, ni original tu hakuna feki lakini ukitaka soko la feki nalo lipo pia.
Baadhi ya mizigo yangu ikiwa ipo katika chumba nilichofikia.
Kama kawaida mambo yakipamba moto.
Wadau chumba changu kilikuwa kiko lafu sana kwa ajili mizigo ilikuwa ni mingi sana.
Hapa nikiangalia camera ya still picture nikipata maelekezo kutoka kwa mtaalam toka Congo (katikati) niliyekutananae huko huko,kwa kweli alinisaidia sana...
Mizigo yangu ikiwekwa sawa na wachina wenye duka hapo hakuna boss wao ndio wauzaji na wao ndio wafunga mizigo,Hawa jamaa wapo makini sana na kazi na ndio maana sikukuu yao ya mwaka mpya wanakaa mwezi mzima bila kufanya kazi yoyote kama muda huu ukienda China utakuwa umepata hasara hakuna duka la shughuli yoyote inayoendelea kwa sasa..
Picha ya pamoja, rafiki yangu Choba na wachina wenye duka.
The greatest naye akipata picha ya kumbukumbu.
Nikikagua vifaa, ukiingia kwenye duka hili ukosi kitu cha video production.
Hapa ni hatari tupu, wewe angalia mwenyewe .
Dolly nimenunua hela nyingi kidogo ni special kwa ajili ya shorts flani hivi ambazo mtaziona kwenye movie mpya ambazo nitawatajia.
Taa mpya pia nimenunua kwa ajili ya kuongeza ubora, hizi ni taa bora sana kwa matumizi yetu.
Upande wa camera.
Duka zima linavyoonekana sijui hata haya maandishi yana maana gani? Kwa ndugu zangu wachina watakuwa wanajua maana yake. Haya ni baadhi tu ya matukio bado mengi nitawaletea na usiku huu nategemea kuondoka kurudi bongo hapa napowablogisha nipo uwanja wa ndege...... Says Ray The Greatest kwa msaada wa http://www.raythegreatest.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment