Saturday, January 14, 2012

MARA YA MWISHO KANUMBA ALIVYOKUTANA NA MAREHEMU MZEE KIPARA KABLA YA KIFO CHAKE:


Kwangu mimi binafsi nitamkumbuka sana Mzee huyu hasa kwa mambo yafuatayo;

1.Kwangu alikuwa kama baba mzazi tena mtoto wa pekee,alinipenda sana nami nilimpenda hii utaiona hata pale alipoumwa nami nikawa nje ya nchi aliuliza mara kwa mara Kanumba hajarudi?Lakini pia kati ya namba za simu alizokuwa amezishika kichwani za wasanii wote wa Kaole nadhani ya kwangu ilikuwa mojawapo hakuitaji kuisave.


3.Alinisisitizia sana Shule na kunitetea hasa pale nilipochelewa mazoezini Kaole kwa sababu ya kuchelewa kutoka shuleni nikiwa secondary,wapo viongozi ambao waliniambia soma kwanza sanaa baadae ila yeye alinitengea mda maalumu mbali na ule wa saa nane bali nilifika saa kumi au tisa na kufanya mazoezi ,Hapa alisisitiza kuwa Sanaa yahitaji Elimu hivyo soma mwanangu.
4.Alipenda sana Ukimya na Upole wangu na hapa aliongea kwa ukari kwamba Usijifanye mpole hapa ukishakuwa staa uanze kuwa kimbelembele,kwa hili nimeendelea kumthibitishia hadi pale mauti yalipomfika hakuwai kuona tofauti yangu kitabia tangu niko Kaole sijulikani hadi nilipojulikana.

5.Alinisihi sana kujiepusha na Ugomvi wowote ule,bali hekima na maarifa walinijaza yeye na marehemu Mzee Pwagu,kuna wakati walinitania wakisema weeee Kanumba ebu tizama mimi na mzee mwenzagu Pwagu tangu ujana wetu hadi sasa hatujawai hata kunyoosheana vidole,vipi nyie vijana mpigane ngumi na kurushiana maneno?siku nikikuona unapigana nakutandika na hii bakora yangu...hapa wote tulichekaa,Jambo hili nililimudu tangu Kaole sikuwai kupigana na mtu yoyote iwe kwa ngumi au kutukanana,Wazee wetu hapa walifanikiwa kutuunganisha kama ndugu walio katika kundi moja kwa upendo,Tizama leo hii hawapo

TUNATENGANA,TUNAGOMBANA, HATUPENDANI,CHUKI ZA WAZI WAZI, TUNAJIKWEZA NA KUJIINUA HATA PASIPOSTAHILI, Hapa Mwenyezi Mungu atusaidie sana. Nitamkumbuka kwa utani wake alipopenda sana kunitania nami nilimtania pia,nilichukua fimbo yake na kuificha wakati akitafuta anagundua nimeficha basi anafoka kidogo ila lengo linabaki palepale UPENDO.Alinibariki na kunipongeza kwa kila hatua nzuri ya kisanaa niliyopiga,Alinitia moyo pale nilipojikwaa,Alinifariji pale nilipoumia,na akafanyika rafiki wa kweli.Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi..amen.
Hapa ni siku niliyomtembelea kigamboni wakati alipoanza kusumbuliwa na matatizo ya miguu mwaka jana.
Nilimpatia kiasi kadhaa cha fedha kwa ajili ya kupata mahitaji mbalimbali hapo alipokuwa.
Ni kawaida yake alipenda kushukuru, kubariki na kukuombea dua.
Pamoja na kwamba miguu ilikuwa inamsumbua lakini alijitahidi kunisindikiza.
Hapo ni stori mbali mbali za hapa na pale..nikiiba hekima na busara za wazee.

Hapa alivyokuwa akinielezea miguu inavyomuuma na jinsi tatizo lilivyoanza.

2.Mzee Kipara ndiye aliyenipokea wakati najiunga Kaole mwaka 2001 na kuhakikisha napata nafasi ya kuwa kundini humo na kufanyiwa interview,kipindi hiki alinisisitiza sana kuwahi na kufanya mazoezi,alinisihi kuacha mzaha na kujibidiisha kundini humo maana Sanaa alijua itanifikisha mbali.

No comments:

Post a Comment