Friday, January 13, 2012

KUELEKEA CHARITY VINTAGE SALE JUMAMOSI HII:

Yaap..Yaap..Yoo, Kuelekea Siku maalumu ya kuuza vile viwalo kwa ajili ya kushangisha pesa zitazosaidia watoto yatima kwenda shule, Jumamosi hii. Mambo yote yameshajipa, nguo zimesharudishwa toka Dry Cleaner na hapa ndio zilikuwa zinapangwa na kupachikwa Tag za bei. Kila nguo zishapangiwa bei yake.... Viatu navyo vishaandaliwa tayari kwa kukuuzia....Kuna nguo za kila aina, Ofisini....B2A...Hadi Abaya. Ni wewe tu na choice yako.

                                                       NASISITIZA:
HII NI CHARITY::: Njoo utuchangie kivyovyote vile kwa kutupatia pesa cash kujinunulia mwenyewe, kumnunulia dada, mdogo wako, au rafiki yako.

MAHALI::: KIKIS FASHION Mikocheni pembeni ya Baclays bank na Engen Petrol Station.

MUDA:::    Saa 4 asubuhi hadi saa moja usiku.

SIKU:::       Jumamosi hii, Tarehe 14.01.2012.

Viko tayari.
Toka Dry Cleaner.
Viatu, vikiwa tayari tayari

Zipo kama hizi B2A mpyaaaaaa, hazijavaliwa kabisa.
Pendaga Abaya wewe..? Just Relax, nazo zipo.
Mtoko sasa, wacha wee.

Zipo Catalogue kibbbaooo, Here's just to expose some.

No comments:

Post a Comment