Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa alitoa sadaka jana kabla ya kuendesha harambee ya ujenzi wa Kanisa la Parokia ya Nyakato Jimbo Kuu katoliki Mwanza.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu wa CCM Mkoa wa Mara, Christopher Mwita Gachuma, katikati, akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa muda mfupi kabla ya kuendesha harambee ya ujenzi wa kanisa, kushoto ni Lawrance Masha mwenye miwani.
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa akihutubia waumini wa kanisa Katoliki Parokia ya Nyakato Jimbo Kuu la Mwanza jana kabla ya kuendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo kubwa kuliko yote Kanda ya Ziwa ujenzi ambao utagharimu kiasi cha shilingi milioni 700. Kanisa hilo litakuwa na uwezo wa kubeba waumini 3000 kwa wakati. Katika harambee hiyo zilikusanywa shilingi milioni 200 ikiwa ni zaidi ya mahitaji ya shilingi milioni 120.
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa mwenye miwani , kulia ni Mkuu wa wilaya ya Nyamagana na kaimu mkuu wa wilaya y Ilemela, Said Amanzi ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo,wa kwanza kushoto ni Raphael Chegeni, mbunge wa zamani wa jimbo la Busega, Mbunge wa zamani wa jimbo la Nyamagana, Lawrance Masha na Mwita Gachuma MNEC, muda mfupi kabla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa Katoliki Parokia ya Nyakato, Jimbo Kuu Katoliki Mwanza.Picha na Mdau Richard Mwaikenda .
No comments:
Post a Comment