Sunday, October 9, 2011

BAADA YA MWANZA, DIAMOND KAZINGUA TENA ARUSHA, ATAPELI PESA ZA SHOO, WACHEZA SHOO WAKE WAKAMATWA, AWA CHANZO CHA GHASIA ZILIZOPELEKEA HASARA YA JUMLA YA MIL.20:

Jeshi la polisi mkoani Arusha linamsaka msanii wa muziki wa kizazi kipya wa jijini Dar es salaam, Nassib Abdul Juma almaarufu kama Diamond (Pichani) kwa tuhuma za utapeli kwa kujipatia kiasi cha Tsh. Mil1.5 na kushindwa kuhudhuria shoo jijini Arusha na hatimaye kusababisha vurugu na uharibifu mkubwa wa mali katika ukumbi maarufu wa Tripple A.
Diamond anadaiwa kuingia mkataba na kampuni ya Arbab MB Entertainment ya jijini Tanga kufanya shoo ijumaa tarehe 8 October 2011 kwa malipo ya jumla ya Tsh. Mil 2.5 na kupokea advance ya Tsh. Mil 1.5 na kuingia mitini kwa kile kinachodaiwa kuchelewa na kuachwa na ndege. Habari zaidi bonyeza hapa: MICHUZI:

No comments:

Post a Comment