Sunday, October 9, 2011

FAMILY DAY AT LIDAZ CLUB KINONDONI DAR:

Watazamaji wakijipa raha kutoka stejini jioni ya leo maeneo ya Lidaz Club katika bonanza la Family Day liloandaliwa na kampuni "tata" ya burudani hapa nchini, Prime Time Promotions na Clouds Media Group.
Mkurugenzi wa kampuni ya Prime Time Promotions, aliyevaa miwani, Juhayna Kusaga, akiwa na baadhi ya rafiki zake na watoto zao wakisherehekea Family Day jioni ya leo katika viwanja vya Lidaz Club jijini Dar.
Palinoga Lidaz.



Uchoraji pia ulikuwepo.
Dogo Aslay anayetamba na ngoma yake ya "Naenda kusema kwa mama" naye alikuwepo kutoa shoo kali kwa mashabiki wake.
Na mvua ikaanza kunyesha na yenyewe ikisherehekea The Family Day pande za Lidaz.
Shabiki akicheza goma la Prakatatumba stejini pamoja na Cabo Snoop (Kushoto) na Meneja wa Cabo Snoop.
Msanii Cabo Snoop kutoka Angola (Kushoto) akiwa Meneja wake stejini wakionesha mambo ya Prakatatumba na Windeck.
Meneja wa Cabo Snoop akimpga mkwara DJ kwamba aendelee kuachia ngoma ya Windeck ili watu wacheze pamoja na msanii huyo kutoka Angola.
Wacheza shoo wa Twanga pepeta wakiwa stejini.
Wakali wa chakachaka walikuwepo pia kuleta ladha katika bonanza hilo jioni ya leo.

No comments:

Post a Comment