Monday, September 5, 2011

FIKIRIA UPANDE WA PILI WA DUNIA,DUNIA YA WENYE UHITAJI,UHITAJI WA USICHOKIHITAJI:

ANGALIZO: Picha zote zinazoonekana katika 'Post' hii hazina uhusiano wowote ule na, aidha, Sherehe, sikukuu, utaifa, wala dini yoyote ile, ni picha zenye lengo la kutoa motisha/hamasa ya kuacha kwa wale wote wanaothubutu kufanya hayo yanaoonekana. Twende kazi.
 
Watu hukaa katika majumba ya kifahari meza zikisheheni kila aina ya matunda nayo kwa mafungu makubwa makubwa.

Wakichinja kila aina ya vitoweo, wapishi katika masufuria makubwa walipika vyakula kwaajili ya furaha yenye nia moja tu, nayo ni kupongezana.

Vyakula vya nafaka kwa mashehena vikapikwa.
Nao hula na kunywa na hata kusaza.
Mara baada ya furaha chakula kingi kilichosalia humwagwa hata kisibakie kwani marufuku kula kiporo.
Kikamwagwa majalalani kama taka.
Chakula chooote hutupwa.
Hayo yakifanyika hebu fikiria upande wa pili wa dunia juu ya ndugu zetu wengine, wakiishi kama ndege kuokoteza.

Dunia ya wenye uhitaji.
Uhitaji wa usichokihitaji wewe.
Mtazame mwana na mama huyo anayenyonyesha.

DON'T THROW FOOD ANY MORE, Kusanya peleka kwa wenye uhitaji, uhitaji wa usichokihitaji.

Let this be remembered.. . each time we throw away Food!
He who said to be the Hungry Boy, he is the Angry Boy;
If we create the HUNGRY boys, we therefore, create the ANGRY Boys.
The result of ANGRY Boys is UNPEACEFUL World.

Don't create ANGRY Boys, Don't contribute to UNPEACEFUL World, Dont't THROW Food Away.

No comments:

Post a Comment