Wednesday, June 13, 2012
SINGLE BOY YA ALI KIBA; NAMBA TATU KWENYE RADIO MAARUFU JIJINI LAGOS-NIGERIA:
Kama unadhani kuwa nyimbo za Nigeria zina umaarufu nchini kuliko nyimbo za Tanzania zinavyojulikana nchini Nigeria, unaweza kuwa wrong!
Ngoma ya Alikiba– Single Boy inabang kinoma nchini Nigeria.
Infact kituo cha radio kinachosikilizwa zaidi kwenye mji mkuu wa kibiashara nchini Nigeria, Lagos, The Beat 99.9 FM kimeuingiza wimbo huo kwenye chart zake.
Wiki hii radio hiyo kupitia ukurasa wake imetweet. “ #AfricanTop10 At number 3, we have “Single Boy” Ft. Lady Jay Dee (@JideJaydee) – Ali Kiba (@AlikibaTZ4Real).”
Kwa taarifa yako tu ni kuwa Beat 99.9 FM – Lagos #1 Hit Music Station! inasikilizwa na asilimia 49 ya ya wakazi wa Lagos wanaofikia milioni 15.
Kwenye page yake ya Facebook ina zaidi ya mashabiki 300,000 na Twitter ina zaidi ya followers 21,600. Hivyo kwa resume hiyo, hii si radio ndogo.
Katika hatua nyingine jana kupitia Twitter, Alikiba amesema yuko mbioni kuachia ngoma nyingine, “Get ready for my new track .its a sexy song in another feelings.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment