Friday, June 15, 2012

KIJANA JACKSON THOBIAS a.k.a KUSH AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA TRENI:


Kijana mdogo wa miaka 17, Jackson Thobias, aliyekuwa akisoma kidato cha nne katika shule ya ESACS Academy, amefariki baada ya kugongwa na treni maeneo ya kwao, Kipawa, aligongwa akiwa anasikiliza muziki kupitia headphone huku aki-chat kwa kutumia simu yake huku akitembea kwenye reli. Pamoja na mlio mkubwa wa treni na juhudi za watu kumpigia kelele kuwa kuna treni inakuja nyuma yake, Jackson hakusikia.

Enzi za uhai wake, marehemu Jackson ndiye aliyeshinda kwenye tokelezeiyer inter-school concert iliyoandaliwa na group ya friends 4 friends mnamo tarehe 12 May 2012, pia alishinda dougie competition wakati 5select event ya EATV ilipotembelea ESACS wiki mbili zilizopita.

Jackson alikuwa kijana mwenye kipaji na ndoto nyingi katika umri mdogo wa miaka 17. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake kwa amani. AMINA.

1 comment:

  1. Mungu ailaze roho ya marehemu mahapa pema pepon amina nasi sisi tutakwenda kwa wakati jina la mungu lihimidiwe daiam
    ramsoict

    ReplyDelete