Sunday, June 17, 2012

LISA JENSEN NDIYE MISS TANZANIA 2012

                Lisa katikati akiwa na wenzake
KIMWANA Lisa Jensen usiku huu ameibuka 
kinara katika shindano maalum la kumsaka
mwakilishi wa Tanzania katka shindano la 
Miss World mwaka huu, lililofanyika kwenye
ukumbi wa 327, Mikocheni, Dar es Salaam.
Shindano hilo, lililoshirikisha washiriki wa 
zamani wa Miss Tanzania ambao hawajawahi 
kushinda, dalili za Lisa kushinda zilionekana 
tangu mwanzo, kutokana na kuwafunika 
washiriki ‘ile mbayaaa’ washiriki wenzake tisa.
Shindano hilo, lilianzia kwa warembo kucheza 
shoo ya ufunguzi kama ilivyo ada ya 
mashindano ya Miss Tanzania, baadaye 
wakapita na vazi la ubunifu, ufukweni na 
kumalizia na vazi la jioni, ambako kote Miss 
Mara wa 2006 alifunika mbaya.
Aliyemfuatia Lisa ni Hamisa Hassan kutoka 
Kinondoni, wakati mshindi wa tatu alikuwa 
ni Pendo Laiser Miss Arusha 2008 na wengine
walioingia tano bora ni Stella Mbuge na Jennifer Kakolaki.
Washiriki wengine ni Glorybayanca Mayowa,
Queen Issa, Christine William, Mwajabu Juma
na Neema Saleh. Shindano hili, linafanyika 
kufuatia kalenda ya mashindano ya Miss Tanzania kubadilika na washindi wa mashindano ya mwaka 
huu ngazi ya awali watashiriki katika shindano
la Miss Tanzania baadaye mwaka huu, kumpata mwakilishi wa Miss World mwakani. 
                                                         














                                   TOP 5
TOP 3
                                                            



























Salha Islael (Miss Tz-2011) akimvalisha
taji Miss Tanzania wa mwaka 2012

Mmaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaah! Salha akimbusu Lisa.

No comments:

Post a Comment