Saturday, April 7, 2012

CHA MWISHO ALICHOKISEMA KANUMBA KATIKA BLOG YAKE KABLA YA UMAUTI KUMFIKA:

"KUSEMA UKWELI INAPOKUJA MAMBO YA KUSAIDIA JAMII NAJITAHIDI KUTOA NINACHOKUANACHO MAANA HAPA HUKUMBUKA MANENO YA MWANDISHI ALBERT PINE.., "What we do for ourselves dies with us, What we do for others and the world remains and is immortal."
Hayo yalikuwa maneno ya mwisho ya Kanumba kuyaweka kwenye weblog yake (Posting) kabla ya kufariki dunia usiku wa kuamkia leo. Alisema maneno hayo baada ya kushiriki kikamilifu katika sherehe za 5th Anniversary ya Tanzania Mitindo House (TMH) zilizoambatana na uzinduzi wa duka/ofisi & Training Center.

Kanumba 'The Great', siku chache kabla ya kifo chake, akiwa katika ofisi za Tanzania Mitindo House (TMH), sehemu ya duka la nguo kutoka kwa Designers mbalimbali.

"TULIOSAPOTI MPAKA KITUO HIKI KUFIKIA HAPA KILIPO SOMA MAJINA HAPO JUU JINA LANGU LIPO HAPO" Aliandika/alisema Kanumba kupitia weblog yake siku ya tarehe 6. April. 2012 kabla ya umauti kumfika usiku wa tarehe/siku hiyo hiyo (Ijumaa ya jana).
Hakika kazi ya Mungu haina makosa, Mungu ametoa na Mungu ametwaa. Ndugu yetu, rafiki yetu, mwigizaji wetu, Super Star wetu, ulale mahala pema peponi-Amina.

No comments:

Post a Comment