Ndugu Zangu;
Ningependa kuwafahamisha kuwa Tamimu amefariki dunia usiku wa kuamkia jumapili na mazishi yalifanyika juzi saa kumi jioni katika makaburi ya Tabata Segerea jijini Dar es salaam.
Kwa niaba ya familia ya ndugu Saidi Tamimu Ally, Caris Blog-The Caris Page, inatoa pole kwa wafiwa wote na shukrani za dhati ziwaendee wale wote waliotoa michango yao ya hali na mali wakijaribu kuokoa maisha ya ndugu huyu, Saidi Tamimu Ally.
Ikumbukwe, wiki kadhaa zilizopita mtandao huu uliweka taarifa ya ndugu yetu Said Tamimu Ally ikiwa na kusudio la kuomba msaada wa matibabu ya ugonjwa wa kansa ya ngozi iliyokuwa ikimsumbua ndugu huyu ambaye pia ni mlemavu wa ngozi (Albino) ambapo kwa sasa ni marehemu.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi, Amina.
No comments:
Post a Comment