Wanamuziki wa Mapacha Watatu, Kalala Junior (aliyebebwa) na Khaleed Chokoraa, wakionyesha uwezo wao jukwaani hapo.
Chokoraa na Halima Kimwana wakishuka kwenye ndege ya Dar Live.
Mwimbaji wa kundi la Super Shine Modern Taarab, Ally Mikidadi, akiwajibika.
Bosi wa TOP Bandi, mwanamuziki TID, akiwajibika.
Dogo Hamidu a.k.a Nyandu Tozi akiwa na Mr Blue.
Dogo Mfaume akiwajibika.
Mr Blu akitoa burudani kwa kila mtu.
Msanii Zuhura akipagawisha mashabiki.
Kundi la Wakali Dancers likitesa jukwaani.
Watoto wakiserebuka ukumbini.
Msanii wa kucheza na kuigiza, Mpella Shaa ‘Kidevu cha Kuku’ akiwa amekaa juu ya chupa jukwaani hapo.
Umati uliokuwa ukumbini ukifuatilia burudani hizo. Picha: Musa Mateja/GPL .
WASANII wa muziki wa kizazi kipya na dansi Bongo, Khaleed Mohamed ‘TID’, Herry Samir ‘Mr Blu’, wakiwa na kundi la Mapacha Watatu ambalo linaongozwa na Khaleed Chuma ‘Chokoraa’, Junior Kalala ‘Kalala Junior’, na Joseph Michael ‘Jose Mara’, na kundi la muziki wa mwambao la Super Shine, usiku wa kuamkia leo wamefanya kufuru ndani ya ukumbi wa kisasa wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam. Wanamuziki hao walivunja rekodi ya mashabiki wengi waliowahi kushuhudia makamuzi kama hayo katika kituo hicho cha burudani nchini.
Shoo hiyo pia ilisindikizwa na makundi mengine kama Wakali Dancers, na wasaniii wengine wa Bongo Fleva wakiwemo Zuhura na Dogo Mfaume na Hejos Band.
No comments:
Post a Comment