Sunday, January 1, 2012

SHAMRA SHAMRA ZA MKESHA WA MWAKA MPYA MAENEO MBALIMBALI:


Saa sita usiku siku mpya tarehe 1.jan/2012 Leaders Club jijini Dar es salaam nchini Tanzania watu waliukaribisha mwaka kwa milipuko ya mabaruti na mafataki hewani.

Time Square huko New York nchini Marekani, Mvua ya maua ikianguka kusherehekea January 1, 2012.
Rais Kikwete naye akisherehekea mkesha wa mwaka mpya kijijini kwao Msoga, Bagamoyo.
Rais Kikwete akisalimiana na baadhi ya wakaazi wa kijiji cha Msoga wilayani Bagamoyo.
 
Fashifashi ziking'alisha anga la kijiji cha Msoga, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani.

Mkesha wa mwaka mpya katika uwanja wa Samora mjini Iringa; Baadhi ya viongozi wa serikali walioambatana na mgeni rasmi wakiwa wamesimama katika kuukaribisha mwaka mpya 2012.

Mkuu wa mkoa Iringa Akihutubia umati wa watu wliohudhuria katika mkesha wa mwaka mpya uwanja wa Samora.



Umati wa watu uliohudhuria katika mkesha wa kuukaribisha mwaka mpya 2012 uwanja wa samora mkoa wa Iringa.
Diamond naye asherehekea mwaka mpya lupango huko huko mjini Iringa baada ya kuwazingua raia kwenye shoo na kumpiga mwandishi wa habari, Francis Godwin wa mjini hapo.
Mwandishi wa habari wa mkoa Iringa, Francis Godwin, akiwa amechaniwa vibaya koti lake na Diamond mara baada ya kumvagaa na kumpiga.
Diamond akiwa chini ya ulinzi wa polisi akitolewa Hotelini na kuelekea kituoni.
Diamond akisimamiwa na mashibiki akilazimishwa kuimba bila ya vyombo.

No comments:

Post a Comment