Wednesday, January 25, 2012

BUNGE: MWALIKO WA WADAU KUTOA MAONI KATIKA MUSWADA WA SHERIA MBALIMBALI ZA BIASHARA "THE BUSINESS LAWS MISCELLANEOUS AMENDMENTS ACT" 2011, PUBLIC HEARING:

YA: MWALIKO WA WADAU KUTOA MAONI KATIKA MUSWADA WA SHERIA MBALIMBALI ZA BIASHARA "THE BUSINESS LAWS (MISCELLANEOUS AMENDMENTS) ACT, 2011"
 (PUBLIC HEARING)

Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara inawaalika wadau wote kwenye mdahalo wa kupokea maoni kuhusu Muswada wa Sheria Mbalimbali za Biashara "THE BUSINESS LAWS (MISCELLANEOUS AMENDMENTS) ACT, 2011". Kikao hicho kitafanyika kesho tarehe 26/01/2012 katika Ukumbi wa Karimjee Dar es SalaamTanzania. Sheria zinazopendekezwa kurekebishwa ni: kuanzia saa 4.00 asubuhi. Lengo la Muswada huu ni kufanya marekebisho katika Sheria mbalimbali kwa lengo la kuboresha mazingira ya kufanya biashara

1. Sheria ya Usajili wa Majina ya Biashara (Sura ya 213)
2. Sheria ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Sura ya 155)
3. Sheria ya Makampuni (Sura ya 212)
4. Sheria ya Bidhaa ya Biashara (Sura ya 85) na
5. Sheria ya Mipango Miji (Sura ya 355)
Nakala za Muswada husika zinapatikana Ofisi ya Bunge iliyopo Mtaa wa Shaaban Robert, Jijini Dar es Salaam, na wahusika wamuone Ndg. Kaboneka (Simu 0755-362852).
Karibuni nyote ili tuweze kuboresha Muswada huu .

Imetolewa na Idara ya Habari,
Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimatifa
DAR ES SALAAM.

No comments:

Post a Comment