Saturday, January 28, 2012

AJALI YA GARI LA POLISI WALIOKUWA KWENYE MSAFARA WA MAKAMU WA RAISI MKOANI TANGA:

Viongozi wa serikali na wananchi wa kijiji cha Nduu, Mombo mkoani Tanga wakitafuta namna ya kuwatoa askari (FFU) mkoani Tanga mara baada ya gari lao lenye namba za usajiri PT 2000 Toyota Landcruiser kuacha njia na kupinduka bondeni wakati wakiwa kwenye ziara ya makamu wa Rais, Dkt Mohamed Bilal iliyotokea jana eneo la Nduu Mombo mpakani mwa wilaya ya Lushoto na Korogwe.
Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mkoani Tanga wakipata msaada wa kuvutwa kutoka kwenye bonde baada ya gari yao kuacha njia na kupindukia bondeni wakiwa kwenye ziara ya msafara wa makamu wa Rais, Dkt Mohammed Bilal, eneo la Nduu-Mombo.
Mmoja wa majeruhi katika ajili hiyo akipata matibabu katika hospitali ya Magunga wilayani Muheza.
Wananchi wa Mombo na viongozi wa serikali wakiangalia ajali hiyo mbaya iliyotokea eneo la Nduu-Mombo na hatimaye kupoteza maisha ya askari wawili na kujeruhi wengine wanne

No comments:

Post a Comment