Thursday, December 15, 2011

MBUNGE WA ILEMELA AKUTANA NA WAENDESHA PIKIPIKI WA JIJINI MWANZA:


Mbunge wa Ilemela Highness Lema akiteta jambo.Uongozi wa Bodi ya Waendesha pikipiki jijini Mwanza leo umekutana na wadau wake, jeshi la polisi na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo mbunge wa Ilemela kwaajili ya kuzungumzia mstakabari mzima wa hali ya waendesha pikipiki.
Changamoto mbalimbali zimejadiliwa suala kuu likiwa ni Uvunjifu wa Sheria, ambao umepelekea kusababisha madhara makubwa kwa jamii hususani vifo kwa madereva wenyewe au kwa abiria ambao wamekuwa wakiwabeba.
Tatizo sugu la rushwa nalo lilijadiliwa kwenye mkutano huo uliofurika madereva wa pikipiki.
Elimu ya usalama barabarani nayo ilitolewa kuelimisha madereva wa pikipiki ili kuendesha kwa usalama kwa kuzingatia kanuni.

Umoja wa madereva pikipiki Mwanza ukisikiliza yaliyomo mkutanoni.

No comments:

Post a Comment