Friday, November 18, 2011

SERIKALI YA TANZANIA NA SERIKALI YA KENYA ZATUMIA DOLA MILIONI 2.2 KUJENGA BARABARA:

Na Ismail Ngayonga
Maelezo Dodoma
17/11/2011
 SERIKALI ya Tanzania na ile ya Kenya zimetumia kiasi cha Dola Milioni 2.2 kwa ajili ya ujenzi wa barabara unaoendelea kati ya  Pangani na Bagamoyo  yenye urefu wa kilometa 178.
Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Pangani (CCM), Salehe Pamba leo Bungeni,, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli alisema barabara hiyo ni muhimu kwa wakazi wa pangani na barabara zilizo ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Dkt. Magufuli alisema hatua za awali za ujenzi wa barabara tayari imekwishafanyika ikiwemo upembuzi yakinifu uliofanywa na kampuni ya Airol Limited kutoka nchini Afrika Kusini.
Waziri Magufuli alisema pamoja na tishio la mdororo wa uchumi uliopo duniani kwa sasa, Serikali ya Tanzania itaendelea kuomba fedha kutoka kwa wafadhili ili kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo ambayo itakuwa kichocheo cha maendeleo katika nchi za Afrika Mashariki.
Alisema tishio hilo la mdororo wa uchumi pia litaweza kuikumba Tanzania, lakini pamoja na matatizo hayo Serikali imepanga kumaliza ujenzi wa barabara hiyo ili iweze kutumika na wananchi wa maeneo hayo.
Katika swali lake la nyongeza Mbunge huyo alitaka kujua mikakati ya Serikali katika kutumia fedha za ndani iwapo mdororo wa uchumi itazikumba nchi tajiri duniani ikiwemo wafadhili wa miradi ya barabara.

No comments:

Post a Comment