Wednesday, November 23, 2011

RAIS JAKAYA KIKWETE KUKUTANA NA VIONGOZI WA CHADEMA:

Rais Jakaya Kikwete
---
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea barua ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ya kuomba viongozi wa chama hicho kukutana na Mheshimiwa Rais kuzungumzia Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011.

Mheshimiwa Rais Kikwete amelipokea ombi hilo kwa furaha kwa sababu ni jambo jema.

Kufuatia kukubali kwake ombi hilo, Mheshimiwa Rais ameagiza mawasiliano yafanyike ili kupanga tarehe mwafaka ya kukutana na viongozi hao wa CHADEMA na kuzungumzia suala hilo.


IMETOLEWA NA:

 
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

 
NOVEMBA 22, 2011

 
DODOMA

No comments:

Post a Comment