Friday, August 19, 2011

DID YOU KNOW ABOUT THESE MOVIE STAR COUPLES FROM NIGER AND GHANA..??


Jamaa anaitwa Ramsey Nouah (Nigeria), ameoa na ana watoto watatu ila mtoto wake wa kwanza alimpata kabla ya kuoa na kwa sasa anaishi nchini Marekani (US), Mkewe anaitwa Emily na amezaa nae watoto wawili yaani Quency na Camili kama unavyoona katika picha hapo juu.

Anaitwa Van Vicker (Ghana), ameoa, jina la mkewe ni Adjoa, wamezaa watoto watatu ambao ni J'dyl, J-ian, na Vj kama unavyowaona katika picha hapa juu.

Anaitwa Desmond Eliot (Nigeria), ameoa, mkewe anaitwa Victoria na mwaka jana walibahatika kupata watoto mapacha.

Anaitwa Majid Michel (Ghana), ameoa tangu mwaka 2004 nchini kwao Ghana na mpaka sasa ana watoto wawili, picha hapo juu ni yeye na mkewe na mtoto wao wa pili.
Anaitwa Omotola Jalade (Nigeria), ameolewa tangu ana miaka 18 na mmewe ni Mr.Mathew Ekehinde,walianza mahusiano yao tangu Omotola akiwa na umri wa miaka 16 kabla hata hajaanza kuigiza, mpaka sasa wana watoto wanne kama wanavyoonekana katika picha.

No comments:

Post a Comment