Friday, July 15, 2011

LOWASA AKILI KUSTUSHWA NA UAMUZI WA ROSTAM AZIZ:

Mbunge wa Munduli, Edward Lowassa (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma walipotaka kupata maoni yake kuhusu uamuzi wa Rostam Aziz kujiuzulu nyadhifa zake za ubunge wa Igunga na ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM hata hivyo Edward Lowassa ameeleza kushtushwa na tukio hilo.

 Hata hivyo, Lowassa ambaye naye amekuwa akitajwa katika orodha ya watu watatu wanaopaswa kuachia nafasi zao za uongozi CCM katika kile kinachoitwa chama kujivua gamba, alipoulizwa kuhusu taarifa za yeye kufuata njia ya mshirika wake huyo alijibu: "Siku ikifika nitatoa uamuzi na nitajibu wakati ukifika."

Lowassa alikuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari katika Viwanja vya Bunge mjini Dodoma, kuhusu alivyopokea uamuzi huo wa Rostam na kama yuko tayari kufuata mfano na njia hiyo ya kujiuzulu nyadhifa zote ndani ya CCM.

Note: To post a comment:
Click 'comment',write your comment in the comment pad,THEN (Select Anonymous profile to hide your name OR Name/URL profile to disclose your name ie Name: (Write your name) and URL: (This is optional)) THEN Click 'Post comment',type the word shown for verification THEN Click 'Post comment'.

No comments:

Post a Comment