Friday, July 15, 2011

UKISEMA WA NINI WENZIO HUSEMA TUTAMPATA LINI, NI BAADA YA NA WAKATI ROSTAM AZIZ ALIPOKUWA ANAJIUZULU:

Pamoja na kwamba Rostam Aziz alikuwa akiongea na wazee lakini Vijana nao hawakusita kuonesha masikitiko yao pale walipofika ghafla na mabango yaliyo na jumbe mbalimbali ukiashiria kwamba bado wanamuhitaji mbunge huyo aliyejiuzulu. Ukisema wa nini wenzio husema tutampata lini.
Vilio vya kwikwi na sauti pia vilitawala pindi Rostam alipokuwa anaachia ngazi kwani licha ya kuandamwa na maneno mengi lakini huenda wananchi wa jimbo la Ingunga mkoani Tabora walikuwa wanafaidika sana na uongozi wake jimboni humo.
 Rostam Aziz (kwenye MIC) akisoma hotuba yake ya kujiuzulu mbele ya wazee na wanachama wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Igunga ambao wengi wao waliangua kilio baada ya kusikiliza tamko lake.

Note: To post a comment:
Click 'comment',write your comment in the comment pad,THEN (Select Anonymous profile to hide your name OR Name/URL profile to disclose your name ie Name: (Write your name) and URL: (This is optional)) THEN Click 'Post comment',type the word shown for verification THEN Click 'Post comment'.

No comments:

Post a Comment