Friday, July 15, 2011

MANCHESTER UNITED; TIMU YENYE THAMANI KUBWA ZAIDI DUNIANI:


The Red Devils Squad - 2010/2011 Season.

Mabingwa wa ligi kuu ya England Manchester United wametajwa na jarida la FORBES kuwa ndio klabu ya michezo yenye thamani kubwa zaidi duniani.

The Red Devils wanatajwa kuwa na thamani paundi billion 1.165 ikiwazidi vilabu tajiri kama Dallas Cowboys na New York Yankees.

Thamani ya United inahusisha timu, uwanja, mapato na mikataba ya udhamini.
Taarifa hizi ni nzuri kwa familia ya Glazer ambayo iliinunua klabu hii kwa £790m in 2005, ingawa bado ina deni la linalokaribia £500.

Mapato ya matangazo ya United yamechangia sana kwa timu hii ku-top the chart, wakiwa wanapata £80m kwa mkataba wa miaka 4 kwa udhamini wa jezi waliosaini na kampuni ya bima ya Aon pamoja na mkataba mwingine Nike wa miaka 13 wenye thamani ya £300m.
 

Real Madrid walishika nafasi ya pili kwa vilabu vya soka wakiwa na thamni ya £900m.
Huku habari nzuri kwa wapenzi wa Arsenal ni baada ya timu yao kushika nafasi ya saba wakiwa na thamani ya £740m. Chelsea walishika nafasi ya 46, na timu nyingine za soka zilizoingia katika top 50 ni Bayern Munich(19), AC Milan(34) na Juventus wakashika nafasi ya 49.

ORODHA YA VILABU 10 BORA VYA MICHEZO VYENYE THAMANI KUBWA DUNIANI:

1. Manchester United £1.165billion
2. Dallas Cowboys £1.13bn
3. New York Yankees £1.06bn
4. Washington Redskins £960million
5. Real Madrid £900m
6. New England Patriots £850m
7. Arsenal £740m
8. New York Giants £734m
9. Houstan Texans £727m
10. New York Jets £708m

Note: To post a comment:
Click 'comment',write your comment in the comment pad,THEN (Select Anonymous profile to hide your name OR Name/URL profile to disclose your name ie Name: (Write your name) and URL: (This is optional)) THEN Click 'Post comment',type the word shown for verification THEN Click 'Post comment'.

No comments:

Post a Comment