Wageni wakipokelewa kwa adabu zote walipowasili kijijini hapo.
Tarehe 26 juni - julai 3 mwaka huu wasukuma wanaoishi Mwanza, katika kijiji cha makumbusho (Bujora) maeneo ya Kisesa, huadhimisha siku ya mavuno wanayoiitwa Bulabo. Siku hii imekuwa maalumu sana na ya kihistoria kwa wasukuma hao kutokana na ugeni wa mwanamuziki Shaggy katika msimu huu wa mavuno na hatimaye kusimikwa uchifu wa kabila hilo.
Shaggy akipata maelezo mafupi kutoka kwa mzee Pius Ng'wangu (Mwenye shati la kitenge) wakati alipofika katika makumbusho ya Bujora.
Mwenyekiti wa bodi ya Serengeti Breweries, Jaji Mark Bomani, akizungumza jambo na Shaggy.
Chifu Charles Kaphipa akizungumza machache kabla ya kumtawaza Shaggy kuwa chifu wa kabila hilo.
Baada ya kutawazwa rasmi sasa...What next..??...Ni furaha tu kwenda mbele.Shaggy akisikiliza kwa makini maneno ya busara kutoka kwa jaji Mark Bomani punde baada ya kusimikwa uchifu wa kabila la kisukuma na wazee maarufu wa kabila hilo.
Baada ya hafla hiyo fupi, Shaggy aliondoka katika viwanja hivyo huku akicheza cheza akifurahia heshima kubwa aliyopewa na wenyeji wa Mwanza ya kusimikwa uchifu wa kabila la kisukuma.
Note: To post a comment:
Click 'comment',write your comment in the comment pad,THEN (Select Anonymous profile to hide your name OR Name/URL profile to disclose your name ie Name: (Write your name) and URL: (This is optional)) THEN Click 'Post comment',type the word shown for verification THEN Click 'Post comment'.
No comments:
Post a Comment