Wednesday, May 25, 2011

MWANZA HEROES YATINGA FAINALI KINYANG'ANYIRO CHA KILI TAIFA CUP:

Wachezaji wa mkoa wa Mwanza 'Mwanza Heroes' wakishangilia ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Ilala walioupata katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha, jana tarehe 24 May 2011. Magoli hayo mawili ya Mwanza Heroes yote yalipachikwa na mshambuliaji 'mviziaji' Jerryson Tegete (dakika ya 45 na 57) yameiwezesha timu hiyo kufika fainali ya mashindano hayo. Goli pekee la mkoa wa Ilala lilifungwa na Bakari Mpakala katika dakika ya 87.

Mwanza Oyeeeee.

Note: To post a comment:
Click 'comment',write your comment in the comment pad,THEN (Select Anonymous profile to hide your name OR Name/URL profile to disclose your name ie Name: (Write your name) and URL: (This is optional)) THEN Click 'Post comment',type the word shown for verification THEN Click 'Post comment'.


No comments:

Post a Comment