Saturday, May 28, 2011

AT LAST,BARCA 3-1 MAN U ON THE FINAL UEFA CHAMPIONSHIP:

Mabingwa wapya wa UEFA Championship, FC Barcelona wakishangilia ushindi wao wa  magoli 3-1 dhidi ya Manchester United. Barcelona wameibuka na ubingwa huo katika mchezo ulipigwa leo usiku (Kwa saa za Afrika Mashariki) katika dimba la Wembley jijini London-Uingereza. Magoli 3 yaliyofungwa na Pedro dakika ya 27, Lionel Messi dakika ya 54 na David Villa dakika ya 69 yameweza kuitengenezea rekodi mpya Barcelona kwa kuwa mabingwa wapya kwa msimu wa 2011/2012 na kuweza kuchukua kombe hilo kwa mara ya 4 sasa. HONGERA FC BARCELONA.

Pedro Rodriquez akishangilia goli lake, goli lililofungua dimba katika mechi hiyo.

Goooo, gooo ...Goooo.. (1-0).

 Lionel Messi akishangilia goli lake, goli la pili kwa Barcelona.

Messi akijaribu kuwatoka wachezaji wa Man U.

 David Villa akishangilia goli lake, goli la tatu kwa Barcelona.

Patrice Evra (Nyuma) na Wayne Rooney wakishangilia goli lao la pekee katika mechi hiyo. Goli lilifungwa na Rooney katika dakika ya 34 ya mchezo akisawazisha goli walilokuwa wanaongozwa.

Note: To post a comment:
Click 'comment',write your comment in the comment pad,THEN (Select Anonymous profile to hide your name OR Name/URL profile to disclose your name ie Name: (Write your name) and URL: (This is optional)) THEN Click 'Post comment',type the word shown for verification THEN Click 'Post comment'.

No comments:

Post a Comment