Thursday, March 28, 2013

IN THE QUEST TO BRING IT BIG FOR TALENTED SOCCER PLAYERS WHO ARE NOT GIVEN A TRIAL CHANCE..., THE PADDY POWER COMPANY GOT THIS TO YELL AT TORRES:

Bango la kumkejeli Fernando Torres likiwa pembeni ya uwanja wa Stamford Bridge. Bango hilo linasomeka ‘FERNANDO. We’ve got an onion bag you can actually find. It’s in the burger van mate. Get your hair net on’ ambayo kwa kiswahili kisicho rasmi linamaanisha 'FERNANDO. Tuna gunia la vitunguu, chukua, liko kwenye gari la burger! Bango hilo liliwekwa na kampuni ya Paddy Power ambayo inadai inafanya kampeni ya kuwaokoa wachezaji wenye viwango lakini wanaozea benchi wakati wanaocheza hawana viwango. Hapa wanamtaka Torres aache mpira kwani umemshinda na aende akauze baga. Bango hilo liliwekwa kwa mara ya kwanza kwenye ukuta wa nyumba ya pembeni ya uwanja wa Stamford Bridge, Chelsea wakaenda kulalamika kwenye halmashauri ya jiji la London. Halmashauri hiyo ikaamuru bango hilo litolewe na likatolewa. Lakini Paddy Power wameliweka tena bango hilo, lakini safari hii kwenye kigari kidogo!

No comments:

Post a Comment