Sunday, July 29, 2012

AY NA JASON DERULO, KIGALI - RWANDA:

Mtanzania AY amezidi kuongeza idadi ya mastaa aliokutana nao mpaka sasa kitu ambacho kimemsaidia pia kupanda ngazi kwenye sanaa anayoifanya, unakumbuka kukutana kwake na Sean kingston ndio kulifanya Romeo Miller na Lamyia kumfahamu? na ndio kilikua chanzo cha mastaa hao wa Marekani kuomba kufanya nae kolabo ya Speak with your body.
Haikufunguka njia moja tu, zipo nyingine kama kolabo na Young Joc alafu kuna kolabo nyingine na mkali wa YMCMB Tyga ambayo iko kwenye line sasa hivi, good news zitakuja soon lakini hayo ni baadhi tu ya mafanikio aliyoyapata baada ya kuanza kukutana na Super Stars.
Jumamosi ya July 28 2012 Ay amekutana nchini Rwanda na Jason Derulo a.k.a mume mtarajiwa wa Jordin Sparks… na walifanya show kwenye stage moja.
Pamoja na hayo yote, Ay alikiri kwamba kwa sasa kwenye show za nje kama hizi anachukua sio chini ya dola za kimarekani elfu kumi ambazo ni zaidi ya milioni 15 za kitanzania, ukubwa wa gharama unatokana na eneo anakokwenda kupiga show pia. What's up Ay, Halla at you boy. Congrats brother....kila la kheri kwa kila jambo. Caris hapaaaaa-Ze DressCode.

No comments:

Post a Comment