Tuesday, June 26, 2012

ULEVI NOOOOOMAAA....:

Walevi watatu (3), wamelewa sana, wakakodi Taxi iwapeleke nyumbani kwao ambapo ni sawa na umbali wa kilometa kumi na mbili na nusu (12.5) kutoka mahali walipo. Baada ya kuingia kwenye Taxi, dereva wa ileTaxi alipowaona wamelewa sana, akawasha gari na kulizima papo hapo halafu akasema: "Tayari tumefika". Mlevi wa kwanza (1) akatoa pesa akampa dereva Taxi, mlevi wa pili (2) akamwambia dereva Taxi, "Thank you", na mlevi wa tatu (3) akampiga kibao kidogo yule dereva Taxi, akamwambia, "Siku nyingine usiendeshe mbio kiasi hichi utakuja kutuuwa".

No comments:

Post a Comment