Wednesday, June 6, 2012

TUMSAIDIE MTOTO HUYU:



Rukia akitaabika na maumivu.

Ndugu wapendwa, mtoto huyu, anaitwa Rukia, ameungua vibaya na maji ya moto huko kwao Luangwa mkoani Lindi. Kwa bahati mbaya wazazi wake ni masikini na wameshindwa kumfikisha katika hospitali kubwa za Ndanda na Muhimbili kama alivyoshauriwa katika zahanati ya kijiji chao.

Hali ya mtoto ni mbaya, na kwa juhudi wadau mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Lindi Press Club, Abdulaziz na ndugu Victor aliye Ruangwa, michango inakusanywa kutoka popote ili kunusuru maisha ya mtoto huyu.

Tunaomba kila mwenye mapenzi mema, atume mchango wake kupitia namba zifuatazo: 0756219342/0713235592 au 0716-483532 au 0715-754494.
Hadi sasa tumepata fedha kidogo ambazo juzi tarehe 4 juni, zimetumika kumsafirisha kwa shida kubwa mtoto huyo na wazazi wake kwenda hospitali ya misheni ya Nyangao ambako amelazwa katika wodi namba 3, kitanda namba 2, lakini hapo hospitali wameshauri kumpeleka hospitali kubwa zaidi kwani hali yake ni mbaya sana.
Changia kwa chochote. Huyu ni mtoto wetu sote.

No comments:

Post a Comment