Saturday, March 3, 2012

KAZI KWENU MNAOPENDA KUTUMIA VYETI VYA SHULE VYA WENZENU:

Hi dada Mange, i believe this finds you well with your family
Naomba unipe nafasi kwenye blog yako ili nipate kushauriwa na wana uturn,naomba wana uturn msinishambulie nishaurini kwasababu yamenifika na sijui la kufanya.
Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 25, nilimaliza form four  miaka kadhaa iliyopita kwa bahati mbaya sikuweza kufaulu kuendelea na kidato cha 5, nilipata division four ya mwisho i have to admit uwezo wangu ulikuwa mdogo darasani,nikakaa one year home bila issue yoyote baadaye kaka yangu ambaye alikuwa chuo mwaka wa 2 akaniambia amenitafutia cheti cha mtu niingie chuo, kweli akanitafutia nafasi CBE nikaanza kusoma certificate ya accounts kwa kutumia cheti cha huyo dada ambaye nilikuwa simjui later nilikuja kufahamu kumbe alikuwa girlfriend wake, basi nikamaliza certificate, nikasoma diploma, mpaka advance diploma,  wakati niko Advance diploma  mwaka wa mwisho kakangu akaoa lakini hakumuoa yule girlfriend wake nayemjua mimi na ambaye natumia cheti chake akamuoa dada mwingine tofauti, kwakweli mpaka leo sijui kwanini hakumuoa yule dada na siwezi kumuuliza, basi yule dada alikasirika sana na akaninyang'anya cheti chake yeye wakati huo alikuwa mwaka wa mwisho Institute of Accountancy Arusha,kwakweli nilichanganyikiwa ila sikujua kama impact yake itakuja kuwa kubwa hivi, nilipomaliza chuo nikapata kazi shirika moja Arusha sasa hapo ndo mchezo ulipobadilika after 6 months wakaniambia nipeleke original certificates zangu, Duuh nilidata nikampigia kaka simu akaniambia omba likizo njoo Dar tudiscuss nikarudi tukahauriana nikaamua niache kazi maana ntapeleka vyeti gani wakati cheti cha form four sina. nikakaa home kama one year my cousin sister akanifanyia mpango nikapata cheti cha kuchonga mtaani akanitafutia kazi Bank moja hapa Dar, nikaanza kufanya kazi sijafikisha hata mwaka last month nikaitwa HR naambiwa nisubmit my original certificates, nikasema ni nini tena hiki, basi nikapeleka kile cheti cha kuchonga na vile vingine original vya chuo but natumia jina la yule dada, after a week nikasimamishwa kazi ili kupisha investigation nikaambiwa nimeforge vyeti na mimi sio mwenye hvyo vyeti, as am speaking to you am just home sijui la kufanya, naona kama kakangu ameniponza ningejua ningerisit by then imagine vyeti vyangu vyote vya chuo vina jina la huyo dada, naomba mnielewe wakati huo nilikuwa mdogo sikujua impact ya kutumia cheti cha mtu but i think my brother did so msinihukumu kwa hilo, nimepoteza 6yrs kusoma with all my effrots amd energy na nilijitahidi sana nikapata lower second na sikuwahi kusupp, i have i feeling huyu dada ananifatilia kila napoenda na kuniharibia, hivi naanzia wapi jamani, nirudi tena kurisit form four, naona siwezi that means another 7 yrs za kurudi shule by then ntakuwa na 32yrs ntazeekea shule jamani, yani sijui hata la kufanya nawaza mpaka nafika mwisho, naishia kulia sipati hata usingizi.ndugu zangu wananishauri nirudi shule nianze moja but nahisi siwezi  kusoma tena, naombeni mnishauri labda naweza pata options hapa ambazo hazitahitaji kutumia muda mwingi
Its me a frustrated lady.
Mama Kenzo email yangu kapuni please.

No comments:

Post a Comment