Friday, May 6, 2011

JINSI BI FAUSTA ALIVYO WAKAWAKA KATIKA SENDOFF PARTY YAKE HAPO JANA - MWANZA:

 Bi Fausta (Kushoto) akigonga cheers na moja ya waalikwa usiku wa jana katika bustani ya Ghand Hall jijini Mwanza.
 Benchi la ufundi lililompika Bi harusi mtarajiwa,Bi Fausta,likijipongeza kwa tukio zima
Raia waalikwa kibao walijitokeza katika bustani hiyo ya Ghandi Hall kumuaga Bi Fausta.

Kwa raha zao.
Stori za hapa na pale huku dada Bale yuko mbaaaaaaaaali.
 Dee tyming, Dee Malosha kama kawa kama dawa, katupia haswaaa.
 Mzee pamba nyepesi (katikati) akiwa tayari kamiminia kama sita hivi za haraka haraka.
 Benchi la ufundi tena, kwa heshima na tahadhima tunawaomba msimame tufanye cheers.
 Sana tu.

 Pale kaaaaaaaati, daah! Kaka Kubingwa na King'asti wake. Happy people.

The One Man Army, man alone, Kala B na King'asti wakiwakawaka.
Hayaaaa...! Raia, welcome to the show.
(And vice versa is true)...., habbbari zenu baaana.
Pamba nyepesi once again, hapa alikuwa tayari bwax mbaya karibu azime (6+2=?)
Mmmmh, wee mkaaaaale kaka mzazi. Ma Alvaro wee, ma Malta wee, ma Maji wee.
Mzee wa vimiminika, thanks for the beverages ilikuwa shangwe sana sector hiyo.
 Daa! Nimemsahau jina ila nae alikuwepo.
Wakiteta jambo.
Caris,The Blogger,ndo kwaaanza kunakucha. Mkononi ana gatepass na Camera iliyofanya shughuli hii.
Akiset Camera.
Camera on set ready for action,mmmh!, na zile swagga sasa.
Festo Kefa,Another Blogger, ndani ya Linen na Kibandiko. 
Wanakamati zamu yao sasa, wakisogea sogea mbele.
 Caris akijivuta kwenye tukio for action.
Akimlia pozi raia wa kumfotoa.
Swagga continues, mithili ya T.I.D akifanya shoo ya 'Zeze'. Hope ze Snapshot ramification was INCREDIBLE..!
Wanakamati wakijitambulisha mmoja baada ya mwingine.

Wacha wee.
Wanakamati wakiwa wamemweka mwali wao kati.
Neno kutoka kwa wanakamati. 
Ze Bloggers, Caris n Kefa
Kaka mzazi na Caris Komba.
Maakuli,mapocho pocho, ma ubwabwa ya rangi.
Ofcourse,wasiokuwepo, they missed out.
Kaka mzazi sasa akifanya "shopping ya tumbo".
Bi harusi wetu alipewa mtihani wa kumsaka 'King'asti' wake alikojificha na hatimaye hapo ndiko alikomfuma.
Baada ya kumpata wake,ving'asti haoo wakisonga jukwaa kuu.
 Hii ni moja ya shoo ya vijana waliobamba vilivyo usiku huo.

Na hii ni shoo ya kaka mlemavu wa miguu, ilifana.
Aii aii,nitamtambuaje "kama anaweza-----kwa vitendo,vitendo."

Katika vitu ambavyo huwezi amini ni hii kitu hii. Ghand hall ni ukumbi maarufu sana uliopo mjini kabisa hapa jijini mwanza na ni miongoni mwa kumbi zinazoongoza kupata sherehe nyingi zinazofanyikia kwenye bustani hii, but the most shame full over the odds out there was found inside the latrine and toilets. Ukiingia humo vyooni kwa muda kama huo wa usiku utakutana na mishumaa kama unavyoonekana mmoja wao hapo pichani,yaani hata bulb moja tu imewashinda daah!, na hicho kidumu sijui cha nini. Kaaaazi kweli kweli.
Caris Komba,am signing out.

Photos by: Caris Komba and Festo Kefa.

Note: To post a comment:
Click 'comment',write your comment in the comment pad,THEN (Select Anonymous profile to hide your name OR Name/URL profile to disclose your name ie Name: (Write your name) and URL: (This is optional)) THEN Click 'Post comment',type the word shown for verification THEN Click Post comment 

5 comments: