Saturday, February 11, 2012

KIPINDI CHA DALADALA CHAHAMIA MWANZA:


Daladala katika mitaa ya jiji la Mwanza.
Kile kipindi cha Daladala kinachorushwa kila siku kupitia ITV kikifanyika ndani ya Daladala ambamo humo abiria hujadiliana masuala mbalimbali yanayozunguka katika harakati za maisha yao ya kila siku, sasa ni zamu ya mkoa wa Mwanza hivyo basi ukikutana na Daladala maeneo ya Nyegezi, Kilimahewa, Pansiasi, Igombe, Igoma, Mabatini, Magu na kwingineko kote panda kisha husika.
Mtangazaji wa kipindi cha Daladala kinachorushwa kupitia ITV Daniel Kijo akisalimiana na mkuu wa mkoa wa Mwanza Erenest Ndikilo, pindi crew ya kipindi hicho ilipodhuru ofisini kwa mkuu huyo jijini Mwanza jana tayari kuanza shughuli zake rasmi kuanzia wiki ijayo siku ya jumatatu.

No comments:

Post a Comment