Thursday, January 26, 2012

WAZIRI WA UJENZI, DKT JOHN MAGUFULI AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA KIVUKO CHA MSANGA MKUU KINACHOGHARIMU SHILINGI 2.8 BILIONI ZA SERIKALI YA TANZANIA:

Waziri Magufuli akiongea na waandishi wa habari baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kivuko cha Msanga Mkuu.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (kushoto) akipata maelezo ya ramani kuhusu ujenzi wa kivuko cha Msanga Mkuu jana kutoka kwa Meneja mradi (mzungu) Peter van Bruggen katika bandari ya Dar es Salaam alipofanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya kukagua maendeleo ya kivuko hicho. (kulia pichani ) na Kaimu Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Mhandisi Marcellin Magesa, pamoja na watendaji wa vijiji kutoka Halmashauri ya Mtwara vijijni waliokuja kuangalia maendeleo ya ujenzi wa Kivuko ambacho kikikamilika kitatoa huduma kati ya Mtwara mjini na Msanga Mkuu. Kivuka kimegharimu shilingi bilioni2.8/za Serikali ya Tanzania
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (Kulia) akipata taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa kivuko cha Msanga Mkuu kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Marcellin Magesa (kushoto)jana jijini katika Bandari ya Dar es Salaam. Kivuko hicho kitakuwa na uwezo wa kubeba watu 100 pamoja na kubeba tani 50 za mizigo kimegharimu shilingi 2,8 bilioni za serikali ya Tanzania, Kupatikana kwa kivuko hicho ni kati ya utekelezaji wa ahadi aliyotoa Rais Jakaya Kikwete kwa wakazi wa Mtwara vijijini, , watakaofaidika na kivuko hicho, pamoja na vijiji vitano vya Namera, Sinde,Mkubiru, Mnete pamoja na Msanga Mkuu yenyewe vyote vipo Mtwara vijijni .
Waziri wa Ujenzi DKT. John Magufuli (alievaa kofia) akifuatiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma ambae vilevilie ni Mbunge wa Mtwara Vijijini Hawa Ghasia (mwenye mtandio) wakiteremka kwenye kivuko cha Msanga Mkuu kinachojengwa katika Bandari ya Dar es Salaam Jan 25,2012 ili kuangalia maendeleo ya ujenzi, Kivuko kimegharimu shilingi 2.8 bilioni za Serikali ya Tanzania.kivuko hicho kitakachotoa hudumu kati ya Mtwara vijijini na Msanga Mkuu kinatarajiwa kukamilika mwezi Mei 2012 na kitakuwa na uwezo wakuchukua watu mia moja pamoja na tani 50 za mizigo,Vilevile wananchi watalipia shilingi mia tatu kwa kuvuka,na wanafunzi wenye unifomu ni bure.
Mafundi wa kiwa kazini wakiendelea na ujenzi wa kivuko. Picha na Mwanakombo Juma-MAELEZO.

No comments:

Post a Comment