Wednesday, January 11, 2012

JUMA NATURE NA MR BEAN (WA MAREKANI) SASA KUTOKA NA SINTA:

Ukimtaja Sinta basi utakumbuka ule uhusiano uliokuwa gumzo sana hapa Bongo mnamo miaka ya 2000 hadi 2004 wakati huo Juma Nature akitoka na mrembo huyu, lakini baadae penzi la wawili hao likaingia dosari.Kwa sasa wanakuja tena pamoja lakini si kimapenzi tena bali ni kwenye upande wa sanaa ya filamu ambapo Sinta ana mpango wa kutoa filamu yake itakayokwenda kwa jina la Sitaki Demu ambapo atamshirikisha mpezi wake uyo wa zamani (Juma Nature) lakini pia atamshirikisha nyota wa vichekesho kutoka nchini Marekani anayefahamika kwa jina la Mr.Bean, mwenyewe alithibitisha kwa sasa yupo kwenye mazungumzo ya mwisho na msanii huyo kutoka kule Marekani na muda wowote atatua hapa nchini kufanya kazi hiyo.Pia alipoulizawa kama ana mpango wa kurudiana na mpenzi wake wa zamani (Nature) alisema kwa sasa hafikirii swala hilo.

No comments:

Post a Comment