Wednesday, January 11, 2012

MLALAMIKAJI ASHANGAA DIAMOND KULETWA MAHAKAMANI NA GX 100:

Gari, GX 100, iliyombeba Diamond ikiwa nje ya mahakama ya mwanzo, mjini Iringa.

Siku chache zilizopita Msanii wa muziki wa kizazi kipya hapa Tanzania anayejulikana kama Diamond alituhumiwa kumpiga na kumharibia vifaa vyake vya kazi mwandishi wa habari na mmiliki wa blog ya Francisgodwin.blogpot.com huko mjini Iirnga na hatimaye mwandishi huyo kufungua kesi mahakamani. Lakini baada ya hukumu ya kesi hiyo kutolewa na hakimu wa mahakama hiyo iliyompa Diamond adhabu ya kifungo cha miezi 6 au kulipa faini ya elfu 80 yani
50 kwa mahakama na 30 kwa mlalamikaji, ambapo Diamond alilipa faini hiyo lakini baadae mlalamikaji alisikika akisema kuwa hajaridhika na adhabu hiyo ya kulipwa elfu 30 kwa kitendo alichofanyiwa kwani alishakataa Tsh. milioni 1.7 alizopewa na Diamond hapo awali na ndio maana aliamua kufungua kesi mahakamani hivyo yeye atakata shauri na kwenda kwenye mahakam za juu zaidi ili kupata uamuzi wa haki wa mahakama na pia alishangazwa kwa kitendo cha mtuhumiwa kuletwa mahakamani na gari aina ya GX 100 badala ya gari la kubebea mahabusu, picha juu ni gari iliyomleta Diamond.

No comments:

Post a Comment