Tuesday, December 13, 2011

LADY JAY DEE AFUNGA MWAKA KWA TUNZO MBILI KUTOKA NCHINI UGANDA:


Mwaka 2011 unafungwa vizuri baada ya Lady JD kutwaa tuzo 2 kutoka nchini Uganda

1.Tuzo ya kwanza ni PAM AWARD -BEST FEMALE TANZANIA
(PAM - Pearl of Africa Music Awards)
Halfa za kugawa tuzo hizo zilifanyika mwezi novemba 2011 jijini Kampala, Uganda.
Zilishirikisha wasanii mbali mbali kutoka nchi za afrika.

Kwa upande wa wanaume alieshinda kutoka Tanzania ni
AY- BEST MALE TANZANIA


Burundi KIDUM alichukua BEST MALE na AZIZA -BEST FEMALE

Best male kwa Kenya ni JAGUAR na best female ni AMANI

Best male Rwanda ni ALPHA na best female ni MISS JOJO


Lady JD amechukua tuzo za PAM kama BEST FEMALE kutoka Tanzania kwa miaka mitano mfululizo

2006/2007/2008/2010 na 2011



2. Tuzo ya pili aliotunukiwa msanii Lady JD ni kutoka DIVA MUSIC AWARDS ambazo pia huwa zinafanyika nchini Uganda, hii ikiwa ni mara ya tatu kwa tuzo hizo kufanyika tangu zianzishwe.

BEST DIVA TANZANIA 2011 - LADY JADEE


Wasanii wengine walioshinda ni SHANEL - Best Diva Burundi

STL MWANGI -Best Diva Kenya


Kutoka Uganda IRYN NAMUBIRU alishinda tuzo 3 Super diva, Diva Collabo na RnB Diva
Wakati JULIANA KANYOMOZI alichukua -Afro Beat Diva.


Mbali na Diva awards, mwanamuziki IRYN pia alishinda tuzo 4 kutoka PAM AWARDS ikiwemo tuzo ya artiste of the year 2011 akiwaangusha Bebe Cool na Jose Gaddafi Chameleon.

No comments:

Post a Comment