Thursday, November 17, 2011

SERIKALI KUJENGA MAHAKAMA KUU KILA MKOA IFIKAPO MWAKA 2013:

Waziri wa Katiba na Sheria Celina Kombani.
Na Ismail Ngayonga Maelezo-Dodoma
SERIKALI katika kipindi cha mwaka wa fedha 2012/13 imekusudia kujenga mahakama kuu katika mikoa yote nchini ili kuwawezesha wananchi kupata huduma za msaada wa kisheria kwa urahisi zaidi.
Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Diana Chilolo, Waziri wa Katiba na Sheria Celina Kombani alisema kupitia mfuko wa mahakama, kipaumbele cha sasa cha Serikali ni kujenga mahakama hizo nchini.
Alisema katika kutekeleza ahadi hiyo, mpaka sasa Serikali imekwisha jenga mahakama hizo katika mikoa ya Shinyanga na Kagera.
Kombani alisema mfuko huo ambao umepitishwa na Bunge mwaka huu na kutengewa kiasi cha Tsh Bilioni 20, katika awamu ya kwanzaya utekelezaji kipaumbele kilitolewa katika usikilizaji wa kesi zilizokuwepo katika mahakama mbalimbali nchini.
Alisema Serikali imepanga kujenga mahakama hizo katika awamu, ambapo mbali na kujenga mahakama kuu mipango mingine iliyopo ni pamoja na ujenzi wa mahakama za mwanzo nchini.
Kuhusu mahakama ya Singida, Waziri Kombani alisema Serikali imepanga kuweka fenicha katika mahakama hiyo ili iweze kutoa huduma kwa wananchi, kwani makusudio yaliyopo ni kuhakikisha kuwa jingo hilo linafanya kazi kama ilivyokusudiwa.
Katika swali lake la Nyongeza, Mbunge huyo alitaka kujua ni hatua gani zinachuliwa na Serikali katika ujenzi za mahakama nchini, ikiwemo mahakama kuu ya mkoa wa Singida.

No comments:

Post a Comment