Saturday, November 12, 2011

PICHA ZAIDI KATIKA VURUGU ZA MWANJELWA - MBEYA NA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM JANA:


Moja ya mabango waliyobeba wamachinga hao.

Wamachinga wakiwazomea polisi eneo la kabwe.
 
Moja ya gari lililobinuliwa na kuwekwa katikati ya barabara ya mbeya tunduma.
Baadhi ya wamachinga wakiwa wamelipindua gari yaina ya toyota na kusimama juu yake huku wakitamka maneno makali kwa polisi na jiji la mbeya kwa kuwanyanyasa katika biashara zao
Wamachinga wakichochea moto wa matairi katikati ya barabara ya mbeya na tunduma.
Nivurugu tupu maeneo ya soweto jijini mbeya.
Askari wa kutuliza fujo naye akiwarushia bomu la machozi wamachinga wanaoandamana.
Nae mwandishi wa Habari hizi Joseph Mwaisango alionja joto ya jiwe baada ya kutupwa ndani ya gari ya polisi kwa kosa la kupiga picha matukio hayo ya wamachinga na polisi  baadaye aliachiwa na kuendelea na kazi yake.
Mmoja wa majeruhi wa risasi za polisi katika vurugu za Mwanjelwa leo, Abel Mwalukali akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mbeya baada ya kupigwa risasi kwenye mkono.
majeruhi wa risasi za polisi katika vurugu za Mwanjelwa leo hii akiwa kapigwa kichwani. Hadi sasa kuna majeruhi wanne wa risasi, wawili kichwani, mmoja kwenye paja na mwingine mkononi.

Kwa habari zaidi juu ya Matukio ya Mbeya Endelea Kubofya Hapa.....>>>>>

CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (UDSM): FFU WALIVYOTAWANYA MAANDAMANO YA WANAFUNZI WA CHUO HICHO:
Barabara ya Kuingilia Chuoni UDSM.
 
Gari ya polisi maarufu kama washawasha ilikuwepo karibu kudhibiti maandamano hayo.
Hapa ni Academic bridge.Wanafunzi wakijadili baada ya kuvurugwa maandamano yao, hata hivyo wameapa kujipanga na kuendelea baadaye. Wanafunzi hao wanaandamana kudai mikopo ya mwaka wa kwanza ambao hadi sasa hawajapewa pesa ya chakula wala malazi.

No comments:

Post a Comment