Sunday, November 6, 2011

MAKAMU WA RAIS DK GHARIB BILAL NA RAIS MSTAAFU WA COMMORO WASHIRIKI BARAZA LA IDD NA SWALA YA KITAIFA KATIKA MSIKITI WA AL FAROUK JIJINI DAR ES SALAAM:



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, wakati akipokelewa alipowasili katika viwanja vya Msikiti wa Al Farouk, Kinondo ni jijini Dar es Salaam leo Novemba 6, kushiriki katika swala ya Idd El Haj iliyofanyika Kitaifa katika msikiti huo sambamba na Baraza la Idd.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, akimpokea Rais Mstaafu wa Comoro, Mohammad  Abdallah Sambi, wakati alipowasili kwenye viwanja vya Msikiti wa Al Farouk, Kinondo ni jijini Dar es Salaam leo Novemba 6, kushiriki katika swala ya Idd El Haj iliyofanyika Kitaifa katika msikiti huo sambamba  na Baraza la Idd. 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, akipokelewa na mmoja wa waumini wa dini ya Kiislam, Asha Baraka, wakati alipowasili alipowasili kwenye viwanja vya Msikiti wa Al Farouk, Kinondo ni jijini Dar es Salaam leo Novemba 6, kushiriki katika swala ya Idd El Haj iliyofanyika Kitaifa katika msikiti huo sambamba na  Baraza la Idd.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya Baraza la Eid El-Haj, baada ya swala ya Idd iliyofanyikaKitaifa  kwenye Msikiti wa Al farouq Kinondoni jijiji Dar es Salaam leo Novemba 6.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wa kwanza (kulia) akishiriki Swala ya Idd El Haj, iliyoswaliwa katika Msikiti wa Al Farouk uliopo Kinondoni jijini Dar es Salaam leo Novemba 6. Mbele ni Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania, Ally Muhidin Mkoyogole, akiswalisha swala hiyo iliyofanyika Kitaifa katika msikiti huo sambamba Baraza la Idd.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, akitoa mawaidha kwa waumini wa dini ya Kiislam baada ya swala ya Idd, iliyofanyika Kitaifa katika Msikiti wa Al Farouk Kinondoni jijini Dar es Salaam leo Novemba 6.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal Wa pili (kulia) Rais Mstaafu wa Comoro,  Mohammad  Abdallah Sambi (kulia) Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania, Ally Muhidin Mkoyogole na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, wakijumuika na waumini wa dini ya kiislam katika swala ya Eid El Haj, iliyofanyika Kitaifa katika msikiti huo sambamba na Baraza la Idd katika Msikiti wa Al Farouk, uliopo Kinondoni jijini Dar es Salaam leo Novemba 6.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waumini wa dini ya Kiislam kuomba dua baada ya swala ya Idd El Haj, iliyofanyika katika Msikiti wa aL Farouk Kinondoni jijini Dar es Salaam leo Novemba 6.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) Ramadhan Rashid Madabida, baada ya kumalizika kwa swala ya Idd iliyofanyika katika Msikiti wa Al Farouk Kinondoni leo Nov 6.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam waliohudhulia swala ya Idd El Haj, baada ya kumalizika kwa swala hiyon iliyofanyika katika msikiti wa Al Farouk uliopo Kinondoni jijini Dar es Salaam leo Novemba 6.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mwilima, wakati akiagana na wageni wake waliomtembelea kwenye makazi yake Oysterbay leo.Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi Ya Makamu Wa Rais.

No comments:

Post a Comment